Habari Mpya

Habari Zote

Archive for 2023


KAGERA

HOFU na huzuni vimefunika Wananchi wa Mtaa wa Omukituri, uliopo Kata ya Kibeta, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, baada ya Mke wa Mwenyekiti wa Mtaa huo, CONCHESTER GERVAZI, kukutwa ameuawa asubuhi ya Juni 13, mwaka huu, huku chanzo cha kifo hicho kikiwa bado hakijajulikana.

Akizungumza na Waandishi wa habari kutoka eneo la tukio Mama mkwe wa marehemu, ANAJOYCE DEUS, amesema usiku wa saa tatu ya Juni 12, mwaka huu, alikuwa amekutana na CONCHESTER ambapo anaeleza kuwa ameshitushwa na taarifa za umauti wake siku ya leo asubuhi



Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, GYPSON GODSON, akiongea kwa masikitiko makubwa kufuatia tukio, amesema marehemu ameuawa karibu na nyumbani kwake na mwili wake umeonekana kupigwa na kifaa butu karibu na eneo la shingo, huku akiwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu hadi pale Jeshi la Polisi litakapokamilisha kazi yake ya upelelezi na taarifa rasmi kutolewa na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Naye Diwani wa Kata ya Kibeta, ANASTELA ALPHONCE, amemtaja Mwenyekiti wa Mtaa huo kuwa ni GERVAZI NYOMO, na kwamba kabla ya tukio hilo wanandoa hao walikuwa wakiishi vyema pasipo na vurugu


- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -