KAGERA HOFU na huzuni vimefunika Wananchi wa Mtaa wa Omukituri, uliopo Kata ya Kibeta, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, baada ya Mke wa ...
KAGERA
HOFU na huzuni vimefunika Wananchi wa Mtaa wa
Omukituri, uliopo Kata ya Kibeta, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, baada ya Mke
wa Mwenyekiti wa Mtaa huo, CONCHESTER GERVAZI, kukutwa ameuawa asubuhi ya Juni
13, mwaka huu, huku chanzo cha kifo hicho kikiwa bado hakijajulikana.
Akizungumza na Waandishi wa habari kutoka eneo la
tukio Mama mkwe wa marehemu, ANAJOYCE DEUS, amesema usiku wa saa tatu ya Juni
12, mwaka huu, alikuwa amekutana na CONCHESTER ambapo anaeleza kuwa
ameshitushwa na taarifa za umauti wake siku ya leo asubuhi
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera,
GYPSON GODSON, akiongea kwa masikitiko makubwa kufuatia tukio, amesema marehemu
ameuawa karibu na nyumbani kwake na mwili wake umeonekana kupigwa na kifaa butu
karibu na eneo la shingo, huku akiwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu hadi
pale Jeshi la Polisi litakapokamilisha kazi yake ya upelelezi na taarifa rasmi
kutolewa na vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Naye Diwani wa Kata ya Kibeta, ANASTELA ALPHONCE, amemtaja
Mwenyekiti wa Mtaa huo kuwa ni GERVAZI NYOMO, na kwamba kabla ya tukio hilo
wanandoa hao walikuwa wakiishi vyema pasipo na vurugu
COMMENTS