Habari Mpya

Habari Zote

Showing posts with label HABARI. Show all posts

Bei ya mafuta ghafi duniani imeendelea 22.7 ikilinganishwa na dola 112.9 zilizorekodiwa Aprili 7, 2026, mabadiliko makubwa katika soko la nishati duniani.


Hata hivyo, kushuka huku bado hakujafikia WaTanzania. Wataalamu wanasema bei za rejareja za petrol na diseli nchini zinaweza kuanza kushuka taratibu wiki zijazo kutokana na mzunguko wa gharama za usafirishaji, bima na tozo za serikali kabla ya kufikia mlaji wa mwisho.


EWURA hufanya marekebisho ya bei kila mwezi tarehe 1. Serikali kupitia Wizara ya Nishati imesema iwapo mwenendo huu utaendelea, basi kuna uwezekano wa kupungua kwa shinikizo la gharama za nishati nchini katika wiki na miezi ijayo.


KAGERA

HOFU na huzuni vimefunika Wananchi wa Mtaa wa Omukituri, uliopo Kata ya Kibeta, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, baada ya Mke wa Mwenyekiti wa Mtaa huo, CONCHESTER GERVAZI, kukutwa ameuawa asubuhi ya Juni 13, mwaka huu, huku chanzo cha kifo hicho kikiwa bado hakijajulikana.

Akizungumza na Waandishi wa habari kutoka eneo la tukio Mama mkwe wa marehemu, ANAJOYCE DEUS, amesema usiku wa saa tatu ya Juni 12, mwaka huu, alikuwa amekutana na CONCHESTER ambapo anaeleza kuwa ameshitushwa na taarifa za umauti wake siku ya leo asubuhi



Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, GYPSON GODSON, akiongea kwa masikitiko makubwa kufuatia tukio, amesema marehemu ameuawa karibu na nyumbani kwake na mwili wake umeonekana kupigwa na kifaa butu karibu na eneo la shingo, huku akiwasihi wananchi kuendelea kuwa watulivu hadi pale Jeshi la Polisi litakapokamilisha kazi yake ya upelelezi na taarifa rasmi kutolewa na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Naye Diwani wa Kata ya Kibeta, ANASTELA ALPHONCE, amemtaja Mwenyekiti wa Mtaa huo kuwa ni GERVAZI NYOMO, na kwamba kabla ya tukio hilo wanandoa hao walikuwa wakiishi vyema pasipo na vurugu


 

KKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye hakufahamika kwa jina Amenusurika na kipigo na wananchi Wenye hasira kali mara baada ya kufanya Uharibifu kwa kuharibu mashine ya Kusaga mahindi ya Mjasiliamali mwenzake kutokana na wivu wa kimaendeleo.



Kijana huyo mkazi wa kijiji cha Nyikonga wilayani Mbogwe Mkoani Geita amenusurika na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali mara baada ya kuvamia nyakati za usiku na kuanza kuharibu mashine ya kusaga mahindi iliyo jirani yake inayotumia mafuta ambapo yeye ameajiriwa katika mashine inayotumia Umeme.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mperwa Sekela amesema kesi hiyo kwa sasa iko mahakamani huku  akitoa wito kwa wananchi kuachana na vitendo vya kujichulia sheria mkononi.

Kwa upande wake mmiliki wa mashine hiyo iliyoharibiwa hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo huku mmiliki wa mashine alikokuwa anafanyia kazi kijana aliefanya uharibifu huo amekiri kutokuwa na ugomvi wowote na jirani yake huku baadhi ya wananchi wakishangazwa na kitendo alichokifanya kijana huyo.

Mpaka sasa kijana huyo yuko chini ya uangalizi wa vyombo vya  Dola katika hatua zaidi za uchunguzi wa Tukio alilofanya.

 BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa soko la wakulima kata Ruanda jijini Mbeya wamedaiwa kukumbatia watoto wanao fanya uharifu hali inayo pelekea kukithiri kwa vitendo vya uwizi ndani ya mtaa huo.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa huo mkutano uliokua unahusu namna ya kuuthibiti uharifu unao fanyika ndani ya mtaa wao.


Wananchi hao wamesema kuwa kuna umuhimu wa kurejesha ulinzi shirikishi ili kuweza kukabiria na vitendo vya uharifu vinavyo fanyika ndani ya mtaa.

Nae mwenyekiti wa mtaa huo ELIMGABI NJIBA ameagiza kuondolewa kwa vijana moja ya nyumba iliyopo mtaani hapo inayo daiwa kufuga vibaka.

Vitendo vya uwizi na udokozi vimeibuka kwa kasi hivi karibuni ndani ya mtaa huo hali iliyo walazimu viongozi wa mtaa huo kufanya mkutano na kupanga mikakati namna ya kukabiliana na uharifu unaofanyika ndani ya mtaa wao.
Serikali imesema kati ya taarifa 533 zilizopokelewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) mwaka 2021, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Felishi ameyasema hayo, leo Novemba 5, 2022 wakati akichangia taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali, (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.


Amesema wapo wanaotuhumiwa na waliobainika na wakachukuliwa hatua kulingana na sheria za utumishi.

“Inawezekana watu wanashangaa kuwaona watu mitaani, lakini yule mtu shauri lake limeshachunguza na tayari limeshafanyiwa kazi na mamlaka zinazohusika,” amesema.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ya mwaka 2021, kati ya taarifa walizopokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), 533, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko. Amesema taarifa 102 za CAG, zilichukuliwa hatua za kinidhamu na kwamba mchakato wa kutuhumiwa umegatuliwa Kikatiba.

“Inawezekana watu wakaonekana mtaani ameshafikishwa kwa muajiri na akatiwa hatiani kwa mujibu wa Sheria za Umma na Sheria ya Fedha za Umma,” amesema.

CHANZO: MWANANCHI

CAG na hoja zake

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewakumbusha wananchi wa kijiji cha Vuchamangofi wanaohitaji kuwekewa umeme gharama zake ni Sh. 27,000 kwa vna sio vinginevyo kama ambavyo wamekuwa wakidanganywa


"Msikubali kutozwa zaidi ya Sh.27,000 kwa sasa umeme sio hanasa, kila mtu anatakiwa kupata huduma hii kwa gharama ya chini kwa sababu serikali imeamua kutoa huduma hii maeneo yote nchini," amesisitiza Chongolo.

Chongolo ameyasema hayo akiwa wilani Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa kwenye mwendelezo wa ziara ya siku tano ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, miradi ya maendeleo na kuhimiza sensa ya watu na makazi

Amesema kuna watendaji wasio waaminifu wanawalaghai wananchi kulipa zaidi ya kiasi hicho.



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua maofisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa mujibu wataarifa iliyotolewa usiku wa Jumamosi, Agosti 6, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus amefanya uteuzi huo juzi Alhamisi Agosti 4, 2022.



Miongoni mwa walioteuliwa kuwa majaji wa Mahakama Kuu ni pamoja na Gabriel Pascal Malata ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Kevin Mhina.

Majaji hao walioteuliwa ambao tarehe ya kuapishwa itatangazwa ni;

1. Kevin David Mhina- kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani

2. Gabriel Pascal Malata-kabla ya uteuzi huu alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali

3. Adrian Philbert Kilimi- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili Mahakama

4. Happiness Philemon Ndesamburo- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

5. Victoria Mlonganile Nongwa- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

6. Obadia Festo Bwegoge- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

7. Ruth Betwel Massam-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

8. Godfrey Ntemi Isaya-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

9. Gladys Nancy Barthy-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

10. Haji Suleiman Haji- kabla ya uteuzi alikuwa Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar

11. Fatma Rashid Khalfan-kabla ya uteuzi alikuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

12. Abubakar A. Mrisha-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Serikali

13. Lusungu Hemed Hongoli-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

14. Monica Peter Otaru-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

15. Kamana Stanley Kamana-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi (Tamisemi)

 16. Hamidu Rajabu Mwanga-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi

17. Marlin Leonce Komba-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

18. Dk Mwajuma Kadilu Juma-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe

19. Dk Cleophas K.K. Morris-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam

20. Asina A. Omani-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

21. Aisha Zumo Bade- kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea

22. Mussa Kassim Pomo-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Taarifa hiyo imesema kuwa tarehe ya kuapishwa majaji hao wateule itatangazwa baaadaaye.


RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na maji katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Amesema anatambua matatizo yanayowakabili kina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu hivyo Serikali itahahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 tatizo la maji nchini linakuwa limekwisha.

Rais Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji wa Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizindua mradi wa maji katika kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya wenye thamani ya Sh2.5 bilioni utakaozalisha maji lita Milioni mbili kwa siku.

 

Amesema katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ifikapo 2025 ilielekeza kutatua tatizo la maji na kwa Mkoa wa Mbeya kuna miradi 50 ambayo imefikia asilimia 95 na ifikapo 2025 tatizo la maji litakwisha kwa asilimia 100.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athon Sanga amesema mradi huo umefikia asilimia 70 ambao utazalisha lita milioni mbili zitakazo ondoa tatizo la maji katika Wilaya ua Chunya.

 

Amesema wizara ina mpango wa kuchimba visima vikubwa vya maji  katika mji wa Makongorosi ili kuondokana na hadha kwa baadhi ya maeneo huku akimpongeza  Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka kwa kutatua changamoto ya maji jimboni kwake kwa kuchimba visima.

 

Kwa upande wake, Mbunge Kasaka amemuomba Rais Samia kusaidia kuboreshwa miundombinu ya barabara kutoka chunya mpaka kijiji cha Itumbi ambako kuna shughuli za uchimbaji wa madini ili kufungua fursa za kiuchumi.

 

Mchimbaji mdogo wa Madini Kata ya Matundasi, Aden Mwakyusa amesema ujio wa Rais Samia ikawe chachu ya changamoto za wachimbaji madini kutatuliwa pamoja na kuhodhi maeneo ambayo yanashikiliwa na wachimbaji wakubwa.

CHANZO MWANANCHI

 

SERIKALI ya kijiji cha Lulembela wilayani Mbogwe Mkoani Geita imewatahadharisha baadhi ya watu wenye tabia ya kuwaficha watoto kisha kuanza kudai fidia kwa wazazi wao kwa kisingizio walikuwa wamepotea.

Kaimu Afisa Mtendaji Wa kijiji hicho PAUL NTAHENGAMA ametoa tahadhari kwa watu wenye tabia hiyo nakwamba wamekuwa wakipata taarifa kutoka kwa wananchi japo hawajabaini juu ya uwepo wa vitendo hivyo kwani wengi wanaowakota watoto hao huwaokota kwa nia njema na si kwa biashara.



kwa mujibu wa maelezo ya wananchi katika Eneo hilo wamedai wimbi la kupotea watoto kwa sasa ni kubwa nakwamba cha kushangaza pindi wanapowapata watoto hao huwalazimu kutoa fidia kuwakomboa kutoka kwa wasamalia wema waliowaokota jambo Ambalo wamehisi huenda kuna biashara ambayo inaendelea. Moja kati ya mzazi ambae amekumbana na changamoto ya mtoto wake kupotea nakulipishwa fidia amesema.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho MAISHA WILLIAM MAGINYA amesema Uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha watu wanaotumia Fursa hiyo ya kuficha watoto kujiingizia  kipato wameendelea kulifanyia kazi ili kubaini uwepo wa vitendo hivyo.

Katika hatua Nyingine Bw William amewataka wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao ili kuondokana na changamoto kama hizo kwakuwa wazazi wengi wamekuwa bize na uzalishaji mali nakusahau malezi kwa watoto.

NA NICHORAS PAUL LYANKANDO

BAADHI ya wafanyabiashara katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani geita  mkoani Geita wamesema sheria kandamizi za ulipaji wa kodi imekuwa kisababishi cha wengi wao kuingia katika vishawishi vya utoaji wa rushwa ili kuendelea na biashara.

Wakizungumza katika moja ya kikao na maafisa wa Mamlaka ya Mapato TRA Wafanyabiashara hao wametoa malalamiko yao juu Sheria kandamizi Ambazo zinawakandamiza wafanyabiashara.



Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara CHARLES MAKANJI amesema TRA wamegeuka kuwa chanzo cha kuwadidimiza wafanyabiashara kwa kuwatoza faini Ambazo haziendani na mitaji yao.

Akitoa Ufafanuzi wa suala la kodi Mwalimu Toa Elimu ya Kodi kanda ya ziwa LUTUFYA MTAFYA amesema wao wanasimamia Sheria na Hawamkandamizi mfanyabiashara hivyo amewaomba wawasilishe kero zao katika Ofisi za mamlaka hiyo na kero zao kutatuliwa haraka iwezekenavyo.

Katika Hatua nyingine akawaomba kutoziogopa Ofisi za TRA badala yake watumie ofisi hizo kama kimbilio la kwanza kutatuliwa kero zao.

NA NICHORAS PAUL LYANKANDO


UONGOZI wa hospitali ya misheni Kaibara, iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara, umetakiwa kubandika gharama za matibabu kwenye mbao za matangazo, ili kuondoa utata unaodaiwa kuwepo hospitalini hapo na kuleta manung’uniko kwa wananchi wanaokwenda kupata huduma ya matibabu katika hospitali hiyo.
Mkuu wa wilaya ya BundaLydia Bupilipili,

Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili, wakati akizungumza na Radio Free Africa, kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo.

Bupilipili alisema kuwa amekuwa akipata malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakidai kwamba gharama za matibabu katika hospitali hiyo ziko juu na kwamba zimekuwa hazieleweki vizuri kwa sababu haziwekwi kwenye mbao za matangazo.

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa wilaya ya Bunda, aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kubandika kwenye mbao za matangazo gharama zote za matibabu ili kuondoa utata huo unaolalamikiwa na wananchi.

 “Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu hospitali ya Kibara, hasa kwenye gharama za matibabu. Sasa kupitia vyombo vya habari ninaagiza kuanzia sasa wawe wanabandika gharama za matangazo kwenye mbao za matangazo ili wananchi wazione” alisema.

Pia, alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikipatiwa ruzuku na serikali, ili iendelee kutoa huduma za matibabu kwa wananchi pasipo gharama, kwa makundi maalumu wakiwemo wazee wanaotambuliwa.


Halikadhalika mkuu huyo wa wilaya ya Bunda, aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutoa lugha zisizofaa kwa wauguzi na madaktari, kwani wanawavunja moyo wa kutekeleza wajibu wao, huku akiwataka wataalamu hao kuwajibika ipasavyo  ikiwa ni pamoja na kuacha vitendo vya kuomba rushwa.
SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa ya usafiri, Nishati ya umeme, maji na usafi wa mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango(kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan(JICA), Hiroshi Kato walipokutana kwa mazungumzo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Hiroshi Kato wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Jijini Dar es Salaam.

Kato alisema kuwa mradi mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni udhibiti wa taka ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya vipaumbele vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma.

Aidha Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo la kilimo hususan kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuwakomboa wakulima.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amelishukuru Shirika hilo kwa kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa mji wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi.

Alisema kuwa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuupanga mji wa Dodoma mapema ili kuondoa changamoto za msongamano wa huduma za jamii kwenye eneo moja kama ilivyo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JICA nchini Tanzania Toshio Nagase, alioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Hiroshi Kato (katikati) walipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.


“Pamoja na umuhimu wa miundombinu ya maji, umeme, usafiri wa mjini, lakini pia tunataka tujenge mapema njia za juu (ring roads) ili kudhibiti msongamano wa magari” alisema Dk. Mpango.



Wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Hiroshi Kato wakifuatiia kwa makini majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato, Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa mradi mwingine wa kipaumbele katika mji huo ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato, karibu kilometa 20 kutoka katikati ya mji huo ili kurahisisha usafiri kwa njia ya anga.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazopata ufadhili mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka Japan kupitia Shirika hilo la Kimataifa la Maendeleo (JICA).

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango(kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya juu (fly over) katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam, upanuzi wa awamu ya kwanza ya barabara mpya ya Bagamoyo (Mwenge-Tegeta) na ufadhili mpya wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Morocco hadi Mwenge.
Kamishina Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Shogholo Msangi akielezea kuhusu masuala ya kodi katika maendeleo ya Taifa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango na  Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Toshio Nagase, pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kufanya kazi kwa bidii katika miradi yote inayopewa na Serikali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa (katikati), akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga (kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.


Akikagua hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni kota, Kwandikwa, amesema Serikali itaendelea kuainisha miradi mingine ili kuhakikisha fedha za Serikali zinaokolewa na kusimamiwa kwa uzalendo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa (katikati), kuhusu hatua zilizofikiwa katika utelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo, jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mnafanya kazi zenu kwa weledi, uzalendo na kukamilisha miradi kwa wakati na kuokoa fedha ambazo zitatumika katika utekelezaji wa miradi mingine hapa nchini”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Muonekano wa mtambo wa kuchakata zege unaotumiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.

Ametoa wito kwa wataalamu wengine kuja kupata mafunzo kwa TBA ambao ni chachu ya utekelezaji wa miradi mingi hapa nchini kwa kuwa wanatumia mfumo wa kisayansi na mitambo yenye kusaidia kupunguza gharama za ujenzi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.

Pia, Naibu Waziri huyo ameushukuru uongozi wa TBA kwa kutoa ajira za vibarua takribani 200 kwa siku katika mradi huo na kuwataka  wafanyakazi hao kuwa waadilifu na waaminifu ili kuwa na sifa za kupata ajira za kudumu.
Muonekano wa baadhi ya vitalu vya makazi eneo la Magomeni Kota zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 35.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kukamilika mradi huo kwa wakati, ubora na kwa gharama nafuu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa, akizungumza na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipowatembelea wakala huo leo, jijini Dar es Salaam.

Amefafanua kuwa mradi huo utakuwa una jumla ya vitalu vitano ambapo vitalu vinne vina majengo ya ghorofa nane na kitalu kimoja kina jengo la ghorofa tisa na hivyo mradi utatoa makazi kwa kaya 656.
Meneja Rasilimali Watu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Gerwalda Luoga, akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani) mara baada ya kikao kazi na Naibu Waziri huyo, jijini Dar es Salaam.

Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi mwakani na utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 20 zote ikiwa ni fedha za Serikali.
MKE wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema angependa kuwajua watu waliomshambulia mumewe, aliyewaamuru wafanye shambulio hilo na sababu za kufanya uovu huo.

Mke huyo ambaye pia ni wakili, Alicia Magabe anasema kuwafahamu watu hao ni muhimu kwa kuwa familia haijui kwa sasa watu hao wanatafakari na kupanga kitu gani baada ya jaribio la kwanza la kumuua kushindikana.

Lissu, mmoja wa wanasiasa wasio na hofu kusema lolote wanaloliamini, alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7 akiwa ndani ya gari lililokuwa limewasili kwenye makazi yake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.

Tangu wakati huo, wakili huyo wa kujitegemea na mwanasheria mkuu wa Chadema, amelazwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya na hadi sasa Jeshi la Polisi halijaeleza kama limeshapata fununu ya waliohusika zaidi ya kujibu kuwa linaendelea na upelelezi kila waandishi wanapotaka kujua maendeleo ya suala hilo.

Na sasa mke huyo wa Lissu na ambaye pia ni wakili, Alicia Magabe anataka kuwajua waliomfyatulia mumewe zaidi ya risasi 30, aliyewatuma na sababu za kuwatuma.

Magabe pia anasema familia yake kwa sasa ipo shakani kwa kuwa hajui hao waliofanya shambulio hilo ambalo linaonekana la kukusudia kumuua, wanatafakari nini na kupanga nini.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi katika Hospitali ya Nairobi, Wakili Magabe alisema Lissu ametumia sehemu kubwa ya ujana wake kupigania masilahi na haki za Watanzania, hivyo angependa kuona haki inatendeka.

“Binafsi nimewasamehe kwa kitu walichokifanya, lakini hiyo haina maana kwamba nisingependa kuona haki inatendeka,” alisema wakili huyo.

“Sitaki kuwe na mkanganyiko baina ya kusamehe na hali ya kutamani kuona haki inatendeka.”

Alisema tukio hilo limemfanya aanze kuamini kuwa kuna watu walitaka kumuua Lissu, lakini hawajafanikiwa na anaamini watu hao wapo, hivyo anahofia usalama wa familia yake.

“Mpaka sasa sijasikia kama kuna uchunguzi wowote umefanyika na sijawahi kusikia watu wamekamatwa,” alisema Wakili Magabe.

“Hivyo nawaza kuwa hayupo salama na mimi kama mke wake sijisikii kama niko salama sana. Nawaza hawa watu watakuwa wanatafakari au wanapanga nini. Hiyo ndiyo hali niliyonayo kwa sasa. Sijui hao watu wako wapi.”

Hata hivyo, Magabe alisema Lissu yuko imara na shambulio hilo halijamrudisha nyuma katika harakati zake za kupigania haki na za kisiasa.
Alisema hilo alilionyesha mara tu alipopata fahamu.

“I have survived to tell a tale, I have lived to tell a tale (nimeepuka kifo ili nieleze jambo) ndivyo alivyosema baada ya kuzinduka,” alisema Wakili Magabe.

Alisema baada ya fahamu kumrejea sawasawa amekuwa akizungumza maneno yanayoashiria kwamba ana ari zaidi.

“Spirit yake ipo very high (ari yake iko juu sana). Si mtu wa kusema kuwa baada ya tukio amekuwa mnyonge, mwoga au ujasiri wake umepungua,” alisema wakili huyo.

“Sijawahi kupata hata kauli yake moja inayoashiria kwamba sasa atarudi nyuma. Kama mke nataka mume wangu apone, tutoke hospitali turudi nyumbani. Lakini wanapokuja viongozi wenzake kutoka Tanzania; wastaafu na wa sasa na hata hapa Kenya, kauli zake zote zinaashiria amekua zaidi kisiasa.

“Anasema ‘kuna siku nitapona na nitaendelea na kazi zangu’ ili kuwatia moyo wanasiasa na wanaharakati.”

Kuhusu mumewe kuendelea na siasa baada ya kupona, Wakili Magabe alisema Lissu ndiye anaweza kulizungumzia suala hilo.

“Mimi nikiwa msaidizi wake wa kwanza, nitakuwa mtu wa mwisho kusema Lissu asifanye analotaka kwa kuwa hata akiyatamka hayatakuwa na nguvu mbele za Mungu,” alisema.

“Binafsi nasema alikuja duniani kwa makusudi. Mungu alimleta duniani kwa sababu na alijua hata kabla hajazaliwa maisha yake yatakuwaje na atafanya nini hapa duniani.
“Sidhani kama kuna binadamu anaweza kuzuia yale ambayo Mungu amepanga. Sitaki kusema kama ataendelea na siasa, hataendelea nazo, yupo kwa kusudi lake.”

Magabe alisema kuna watu wanapigwa risasi moja na wanafariki dunia, lakini Lissu alipigwa risasi 16 za moto ambazo zilipita kwenye mwili wake na anaendelea kuishi.

Alisema anafarijika kuona Lissu yu mzima kwa kutumia nguvu za watu wote ambao kwa namna moja au nyingine wanapenda aishi, akianzia na waliochanga fedha, 

waliomtolea damu, walioomba, waliomnyanyua, waliomtibu mara ya kwanza na wanaoendelea kumtibu.

“Hatujawahi kuwa peke yetu na nimegundua kumbe kupigwa risasi kwa Lissu ni tukio ambalo limewagusa Watanzania na mataifa mengi na wapo tayari kusaidia,” alisema mwanamke huyo.

“Hii ni kwa kuwa ametumia ujana wake kupigania masilahi na haki za Watanzania.”
Magabe alisema risasi zilizompata Lissu ziliharibu zaidi mifupa, tishu zilizo karibu na mifupa ya mguu wa kulia na mikono, lakini hakuumia kwenye neva, mishipa mikubwa ya damu, ya fahamu au ogani.
“Madaktari wanasema risasi zilikuwa zinakwepa maeneo muhimu. Ni kitu ambacho hawajawahi kukiona,” alisema.
“Hapa kuna mshipa mkubwa wa damu, lakini risasi imepita pembeni. Walikuwa wanashangaa inawezekana vipi risasi nyingi zikaingia lakini zikakwepa maeneo muhimu.”
Alisema madaktari wamemweleza Lissu kuwa ataendelea kuimarika lakini itachukua muda kabla hajapona na kuweza kutumia viungo vyake vyote kama kawaida.
Mama huyo alisema awamu ya kwanza ilikuwa kumtibu majeraha na ya pili ni kumjengea uwezo wa kutumia viungo vyake ili baadaye aweze kusimama na kurudi katika hali yake.
Magabe alisema ilichukua mwezi mmoja Lissu kutoka ICU na hakuweza kumhudumia kwa ukaribu kutokana na masharti ya chumba cha uangalizi maalumu.
“Kila siku naamka kama nakwenda kazini. Lazima niamke asubuhi kuja hospitali kisha narudi usiku nyumbani. Siruhusiwi kulala hapa,” alisema.
Simulizi ya siku ya tukio
Magabe alisema siku ya shambulio alikuwa ametoka Kerege wilayani Bagamoyo na alipanga kukutana na rafiki yake eneo la Mpiji, Bunju.
“Saa 6:30 nilifika kwake, akaniambia lazima nipate chakula cha mchana, baada ya chakula nilimwambia nipumzike kwenye kochi,” alisema.
“Baada ya dakika 25 akaniamsha akaniambia Alicia amka ukilala sana mchana huu usiku unaweza usipate usingizi,” alisema.
Alipoamka aliwasha simu zake na kukuta ujumbe usemao, “hello sister, kuna taarifa inazunguka sina hakika kama ni ya kweli. Kama kweli pole sana dada yangu.”
Alisema moja kwa moja wasiwasi ulimjia kwamba huenda mumewe amekutwa na jambo baya, alisema alichowaza awali huenda amepata ajali na ndipo akamuomba rafiki yake ampigie mtu huyo simu kujua zaidi kuhusu ujumbe huo.
“Niliingia kwenye magroup ya Whatsapp ya Chadema nikakutana na hiyo taarifa. Nilipiga kelele kwa nguvu, rafiki yangu aliniuliza umeona nini nikamwambia kuna ujumbe huu,” anasema na kumpa rafiki huyo simu asome ujumbe huo uliosema “Tundu Lissu amepigwa risasi.”
“Nilianza kuwaza yupo hai au amekufa. Niliwaza nifanye nini nikamwambia nataka kwenda nyumbani. Huko niliamini kuwa ningewaza kwa utulivu nini cha kufanya.”
Anasema baadaye simu zilianza kuingia mfululizo na ndipo alipoamini kuwa habari hizo ni za kweli.
“Nilimpa jukumu hilo (la kupokea simu) kwa sababu ni rafiki yangu wa karibu tangu sijaolewa,” alisema.
Baadaye waliingia kwenye gari na yeye kuanza kuendesha huku rafikiye akizungumza na waliokuwa wakimpigia simu.
Magabe alisema baada ya kuiingia mtaa wa nyumbani kwake, aliona vijana wanamwangalia katika namna ambayo ilionyesha kuna kitu wanakijua. “Mwonekano wao ulikuwa tofauti wananiangalia kwa huruma, kwa mshangao. Wanatamani waongee,” alisema.
Anasema nyumbani aliwakuta shemeji zake wawili na mtoto wa baba yake mdogo, lakini alishindwa kuingia ndani na badala yake alikaa bustanini.
“Nilipigiwa simu na watu waliokuwepo hospitali na wakaniambia ni kweli amepigwa risasi, lakini yupo hai. Walinitaka nitulie mpaka nitakapopewa taarifa nini cha kufanya,” alisema.
Alisema mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimweleza nini cha kufanya kwa wakati huo.
Alisema baadaye aliambiwa Lissu angepelekwa Nairobi na hivyo aende uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya Dodoma na baadaye Nairobi.
Aliondoka na kaka yake na marafiki wa karibu, lakini alipigiwa simu na kutakiwa kushuka kwa kuwa muda haukuwa rafiki.
“Nilipanda bodaboda,” alisema.
“Wale vijana walikimbiza sana na ilikuwa ni mara ya kwanza kupanda pikipiki Dar es Salaam. Niliogopa na kusali Mungu anisaidie kufika uwanja wa ndege salama.”
Alipofika Dodoma ndipo alipomuona kwa mara ya kwanza Lissu tangu apate taarifa za shambulio.

“Baada ya dakika chache akaja akiwa kwenye kitanda kutoka chumba cha upasuaji. Kwa kumuangalia nilijua ameumia sana hakuwa anajitambua,” alisema
MAADHIMISHO ya Siku ya Takwimu Afrika yatafanyika leo tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya alisema maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika.

Ruyobya alisema kuwa kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora"

"Kaulimbiu hii inalenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote nchini na  Afrika kwa ujumla", amebainisha Ruyobya.

Ruyobya alifafanua kuwa matumizi sahihi ya Takwimu za Uchumi yanaiwezesha Serikali kutunga sera na kutathmini programu mbalimbali kama vile Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP-II), Agenda ya Dunia ya Mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Agenda ya Afrika ya Mwaka 2063.
 
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
"Progaramu zote hizi, zina lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha kuwa, kuna upatikanaji wa Huduma za afya, Elimu, Miundombinu ya umeme na barabara, Mawasiliano, Utunzaji wa mazingira pamoja na Utawala bora", amesema Ruyobya.

Jumla ya washiriki 200 kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau mbalimbali wa takwimu nchini wanatarajiwa kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo.


Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Novemba ambapo kwa mwaka huu, Tanzania itaadhimisha siku hiyo kesho tarehe 20 Novemba, 2017.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi 10,460.
Lengo la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.

Dk. Mpango alisema kuwa Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri  na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013 hadi sasa.

“Takwimu zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dk. Mpango.

Alisema pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi unavyokua hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dk. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
“Nimefurahi kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kupitia zoezi hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana wapata 620 katika maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dk. Mpango.

Aliwaasa wadadisi hao kufanyakazi zao kwa umakini na weredi mkubwa ili takwimu zitakazopatikana ziwe sahihi na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuvuruga zoezi hili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dk. Khatibu Kazungu akimkaribisha  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) kufunga mafunzo ya Wadadisi, na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, Mjini Dodoma.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa alieleza kuwa ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi utafanyika katika maeneo 754 yaliyochaguliwa kitaalamu kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.

“Utafiti huu utakuwa wa saba tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961, ambapo tafuti nyngine zilifanyika 1969, 1991/92, 2001, 20117 na mwaka 2011/12” aliongeza Dk. Chuwa.

Alisema kuwa utafiti huo mpya utafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ijulikanayo kama Survey Solution (CAPI) na kwamba matokeo ya awali ya utafiti huo yanatarajiwa kutolewa ndani ya miezi sita ijayo ili nchi iweze kufahamu kiwango cha umasikini uliopo katika jamii hivi sasa baada ya kufanyika kwa utafiti kama huo miaka mitano iliyopita.

“Utafiti wa mwisho uliofanyika mwaka 2011/2012 uliotumia karatasi uligharimu shilingi bilioni 20 lakini kwa kutumia teknolojia mpya, utafiti huu utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 10 pekee” alisisitiza Dk. Chuwa.

Dk. Chuwa alisema kuwa anaamini matokeo ya utafiti huo yatakuwa chachu ya kupata takwimu za msingi kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa program mbalimbali za kitaifa na kimataifa zenye kulenga kupunguza kiwango cha umasikini nchini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu ya TEHAMA


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dk. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara utakao gharimu shilingi bilioni 10, wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.


Baltazar Kibola alisema kuwa watatoa ushirikiano wakutosha kwa wadadisi hao katika ngazi zote kuanzia Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Kata, Vijiji na Vitongoji ikiwemo kufanyia marekebisho vitendeakazi vya kukusanyia takwimu hizo vikipata hitililafu ili azma ya Serikali ya kupata takwimu sahihi itimie kama ilivyopangwa.

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -