Serikali imesema kati ya taarifa 533 zilizopokelewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi M...
Serikali imesema kati ya taarifa 533 zilizopokelewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) mwaka 2021, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Felishi ameyasema hayo, leo Novemba 5, 2022 wakati akichangia taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali, (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.
Amesema wapo wanaotuhumiwa na waliobainika na wakachukuliwa hatua kulingana na sheria za utumishi.
“Inawezekana watu wanashangaa kuwaona watu mitaani, lakini yule mtu shauri lake limeshachunguza na tayari limeshafanyiwa kazi na mamlaka zinazohusika,” amesema.
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ya mwaka 2021, kati ya taarifa walizopokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), 533, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko.
Amesema taarifa 102 za CAG, zilichukuliwa hatua za kinidhamu na kwamba mchakato wa kutuhumiwa umegatuliwa Kikatiba.
“Inawezekana watu wakaonekana mtaani ameshafikishwa kwa muajiri na akatiwa hatiani kwa mujibu wa Sheria za Umma na Sheria ya Fedha za Umma,” amesema.
CHANZO: MWANANCHI
COMMENTS