BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa soko la wakulima kata Ruanda jijini Mbeya wamedaiwa kukumbatia watoto wanao fanya uharifu hali inayo peleke...
BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa soko la wakulima kata Ruanda jijini Mbeya wamedaiwa kukumbatia watoto wanao fanya uharifu hali inayo pelekea kukithiri kwa vitendo vya uwizi ndani ya mtaa huo.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa huo mkutano uliokua unahusu namna ya kuuthibiti uharifu unao fanyika ndani ya mtaa wao.
Wananchi hao wamesema kuwa kuna umuhimu wa kurejesha ulinzi shirikishi ili kuweza kukabiria na vitendo vya uharifu vinavyo fanyika ndani ya mtaa.
Nae mwenyekiti wa mtaa huo ELIMGABI NJIBA ameagiza kuondolewa kwa vijana moja ya nyumba iliyopo mtaani hapo inayo daiwa kufuga vibaka.
Vitendo vya uwizi na udokozi vimeibuka kwa kasi hivi karibuni ndani ya mtaa huo hali iliyo walazimu viongozi wa mtaa huo kufanya mkutano na kupanga mikakati namna ya kukabiliana na uharifu unaofanyika ndani ya mtaa wao.
COMMENTS