· Yamo kisukari, saratani, presha, hamu ya tendo MMEA wa bamia uzaao matuda yanayoliwa, ni zao linalostawi karibu maeneo yote ...
· Yamo
kisukari, saratani, presha, hamu ya tendo
MMEA wa bamia uzaao matuda yanayoliwa, ni zao
linalostawi karibu maeneo yote hapa nchini, ingawa hustawi na hupedwa zaidi na
watu wa ukanda wa Pwani. Huliwa kama mboga kwa matunda hayo kupikwa
yakichanganywa na aina nyingine ya mboga kama vile nyama.
Watu wa ukanda wa Pwani hutumia bamia kwa
kuikatakata vipande vidogo na kuchanganya vipande hivyo na majani ya maboga, magadi kisha kupika pamoja na
kupata mboga iitwayo mlenda au hombwe kwa watu wa pwani ya mkoa wa Tanga.
Kwa bahati mbaya sana walaji wengi hawajui umuhimu
wake kifya kama anavyobainisha Mtaalamu na Mkufunzi wa Chuo cha Tiba na Uuguzi
( IMTU) cha jijini Dar es salaam, Dk. Daniel Elifariji Mtango.
Mtaalamu huyo wa kitengo cha Afya na Jamii Chuoni
hapo, anasema tunda la bamia lina vitamini A na B ambavyo huimarisha macho kutokana
na virutubisho hivyo kusheheni kiasi
kingi cha protini ukilinganisha na lishe nyingine inayotokana na mimea.
Kama hiyo haitoshi, viini lishe vilivyomo husaidia kuwaokoa
watoto wenye tatizo la utapiamlo, isulini kufanya kazi
hivyo kuwaondoa watu katika hatari ya ugonjwa wa kisukari kwa kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.
Zinapoliwa kwa usahihi, huongeza kinga za mwili kwa
watoto na watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka na kuwa kwenye hatari ya
kuambukizwa Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababishwa na kushuka
kwa kinga ya mwili, anasema.
Akifafanua zaidi, Dk. Mtango anasema, maji ya bamia husaidia
kuzuia magonjwa ya moyo kwa kuifanya mishipa ya damu kufanya kazi vizuri
kutokana na maji yake kuwa uwezo wa kuondoa lehemu kwenye kuta za mishipa ya
damu.
“Lehemu zisipoondolewa kwenye mishipa hiyo
husababisha msukumo wa damu kwenda vibaya na kuwa chanzo cha maradhi ya shinikizo
la damu. Kwa hiyo tunaona ni kwa jinsi gani ambavyo mmea huu ulivyo muhimu
katika lishe na kudhibiti magonjwa ambayo wakati mwingine hayawezi kutibiwa
hapa nchini. Hivyo bamia inaweza kupunguza idadi ya watu kwenda India kutibiwa
maradhi ya moyo,”anasema,
Faida zingine za ulaji wa bamia ni kuzuia tatizo la watoto kupasuka uti wa
mgongo au mgongo waz, kumsaidia mama mjawazito pamoja na mtoto tumboni kuwa na afya
na baada ya kujifungua.
Hutibu tatizo la kuchoka bila sababu, zaidi kwa watu ambao wana msongo wa mawazo ambao
mtaalamu anashauri kundi hilo kula kwa wingi bamia kwani huleta matokeo ya
haraka na kufanya afya zao kuimarika zaidi na kuwafanya wawe na amani, furaha muda wote.
Faida nyingine, hutibu vidonda vya tumbo na
kuthibiti bakteria wasababishao matatizo
hayo na kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo, huongeza kiwango cha
uzalishaji wa damu kwa wingi mwilini.
Huimarisha nywele na kuzifanya ziwe na muonekano
mzuri pamoja na kufanya utumbo mpana kubaki katika ulaini wa asili yake na kukinga mtumiaji dhidi ya saratani ya utumbo mpana (large intestine).
Pia hufanya mfumo wa usagaji wa chakula kuwa mzuri
na hivyo kupunguza maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa kutokana na majimaji
ya bamia hulainisha choo kama ilivyo papai na ndizi mbivu. Pia huongeza hamu ya
tendo la ndoa.
MATUMIZI:
·
Mlaji anaweza kupika bamia kama mboga kisha
kuchanganya na chakula kingine na kula kama mlo. Vyakula hivyo vinaweza kuwa, uji,
mchuzi, na vingine.
·
Matumizi mengine ni mtumiaji anatakiwa
kukatakata bamia vipande vidogovidogo baada ya kuoshwa kwa maji safi na salama.
Loweka kwenye maji kwa dakika kadhaa vipande hivyo kulingana na uwingi wa
vipande vyenyewe ili kupata juisi.
·
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha juisi
ya bamia sawa na gramu 100. Au unaweza kula vipande hivyo vibichi vilivyojazwa
kwenye kikombe cha ujazo huo .
·
Inashauriwa kuwa watoto wadogo wapatiwe zikiwa zimepikwa. Fanya hatua hizo tatu kwa mfululizo na matokeo
yake hujitokeza kuanzia juma la tatu au kabla.
Anatoa ushauri kwa wakulima kulima zao hilo kwa wingi
kutokana na faida hizo za kiafya na kukifanya kilimo chao kuwa na tija.
Ni zao
linalokomaa kwa muda mfupi na hukabiliana na hali zote za hewa. Pia jamii kula
kwa wingi bamia ili kupunguza matatizo ya kiafya ambayo baadhi yake ameyaanisha katika makala
haya.
COMMENTS