WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watan...
WATUMISHI wa
kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha
huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi
katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine
Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile |
“Tuna malengo ya
kuwa na watumishi wa hada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na
kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi
95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dk. Ndugulile.
Amesema kuwa
wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali
watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka
hivi sasa.
Mbali na hayo Dk.
Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia
Wizara ya afya imetoa shilingi milioni
700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.
“Tumetoa milioni
700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa
ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni
300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba Dk. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu
wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa
wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.
“Wahitimu
waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa
kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika
taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema.
Mbali na hayo
msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa
fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa
ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye
masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.
COMMENTS