SHIRIKA la utangazaji Nchini Zimbabwe (ZBC) limesema Makamu wa zamani wa rais wa nchini humo Emmerson Mnangagwa, ambaye kufutwa kwake kazi ...
SHIRIKA
la utangazaji Nchini Zimbabwe (ZBC) limesema Makamu wa zamani wa rais wa nchini
humo Emmerson Mnangagwa, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa
kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa.
Emmerson Mnangagwa |
Mnangagwa,
ambaye alitorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo
Jumatano nchini humo ambapo kuondolewa kwake kwake madarakani kulisababisha
chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala
wa miaka 37 wa Mugabe.
Taarifa
hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane:
Katika
barua yake Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu makabidhiano ya
uongozi kwa njia ya amani na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.
Msemaji
wa Zanu-PF alisema kuwa Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika
kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
COMMENTS