Habari Mpya

Habari Zote

Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts


 

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha CNL Agathon Rwasa amesema kupunguzwa kwa mikoa haitakuwa suluhu ya migogoro ya uchaguzi nchini.

NA: BUKURU ELIAS, RWASSA

Picha kutoka BBC SWAHILI



Uwanja wa michezo unaobeba watu 60,000 ulijaa huku raia wa Zimbabwe wakitaka kushuhudia kuapishwa kwa rais mpya.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUwanja wa michezo unaobeba watu 60,000 ulijaa huku raia wa Zimbabwe wakitaka kushuhudia kuapishwa kwa rais mpya.
Kuapishwa kwa bwana Mnangagwa kunafuatia kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe baada ya kuwa mamlakani kwa takriban miaka 37Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKuapishwa kwa bwana Mnangagwa kunafuatia kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe baada ya kuwa mamlakani kwa takriban miaka 37
Bwana Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa Kwnaza ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu hatua iliosababisha jeshi kuingilia kati na kumshinikiza Mugabe kujiuzuluHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa Kwnaza ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu hatua iliosababisha jeshi kuingilia kati na kumshinikiza Mugabe kujiuzulu
bwana Mnangagwa, ambaye alilitoroka taifa hilo alirudi kutoka mafichoni siku ya Jumatano tarehe 21 NovembaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionbwana Mnangagwa, ambaye alilitoroka taifa hilo alirudi kutoka mafichoni siku ya Jumatano tarehe 21 Novemba
Rais mpya na mkewe AxiliaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais mpya na mkewe Axilia
Bwana Mnangagwa amekuwa katikatiu ya urtawala wa Mugabe kwa takriban miaka 37Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Mnangagwa amekuwa katikatiu ya urtawala wa Mugabe kwa takriban miaka 37
Mkuu wa jeshi jenerali Constantino Chiwenga, mtu aliyeongoza mapinduzi ya Robert Mugabe akitazama kuapishwa kwa MnangagwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMkuu wa jeshi jenerali Constantino Chiwenga, mtu aliyeongoza mapinduzi ya Robert Mugabe akitazama kuapishwa kwa Mnangagwa
Bwana Mnangagwa anashirikishwa na wengi na mabaya yaliofanyika chini ya utawala wa Zanu-PfHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Mnangagwa anashirikishwa na wengi na mabaya yaliofanyika chini ya utawala wa Zanu-Pf
Katika hotuba yake alimsifu mtangulizi wake Robert MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKatika hotuba yake alimsifu mtangulizi wake Robert Mugabe
Pia aliahidi kuwatumia raia wote wa Zimbabwe , sio wanachama wa Zanu Pf pekee.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPia aliahidi kuwatumia raia wote wa Zimbabwe , sio wanachama wa Zanu Pf pekee.
Viongozi kutoka mataifa jirani ya Zimbabwe walihudhuriaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionViongozi kutoka mataifa jirani ya Zimbabwe walihudhuria
Alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi , usalama na amekuwa na uhusiano wa karibu na JeshiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAlikuwa waziri wa zamani wa ulinzi , usalama na amekuwa na uhusiano wa karibu na Jeshi
Jeshi liliingilia kati na kumng'atua mamlakani Robert MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJeshi liliingilia kati na kumng'atua mamlakani Robert Mugabe
Umati mkubwa wa watu ulifurahia wakati wa kupigwa kwa mizingia 21 kama heshima ya kumkaribisha rais mpya huku ndege za kijesh zikiwa anganiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUmati mkubwa wa watu ulifurahia wakati wa kupigwa kwa mizingia 21 kama heshima ya kumkaribisha rais mpya huku ndege za kijesh zikiwa angani
Raia wengi wa Zimbabwe waliunga mkono hatua ya jeshi ya kuingilia kati kumuondoa MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRaia wengi wa Zimbabwe waliunga mkono hatua ya jeshi ya kuingilia kati kumuondoa Mugabe
SHIRIKA la utangazaji Nchini Zimbabwe (ZBC) limesema Makamu wa zamani wa rais wa nchini humo Emmerson Mnangagwa, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa.
Emmerson Mnangagwa

Mnangagwa, ambaye alitorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini humo ambapo kuondolewa kwake kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Mugabe.

Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane:
Katika barua yake Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu makabidhiano ya uongozi kwa njia ya amani na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.


Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
SPIKA wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters limemnukuu Jacob Mudenda hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake huku Spika wa bunge akisema kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Mugabe ambaye ameingia madarakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980 alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka madalakani wiki hii.

Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake huku sababu za kumtaka ang’atuke zikiwa ni baada ya kumfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.

Hatua hiyo ilionekana na wengi kama njama ya kumrithisha mkewe na kusababisha viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizini.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala wa kiongozi huyo.

Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.

Ubalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao kwakile kilichodaiwa kuwa ni wakati wa mabadiliko.

Kwa mujibu wa Mwanaharakati wa haki za Binadamu Linda Masarira akiongea na BBC ninafuraha sana leo kwa sababu nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha yangu.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua hiyo kikisema kuwa Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.

''Na sasa kwenda mbele ni wakati wa upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na serikali inayowajali raia wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe''.
MCHAKATO wa kumstaafisha Rais Robert Mugabe umeanzishwa na Spika wa Bunge Jacob Mudenda kusoma sheria na kanuni namna ya kuendelea na shughuli hiyo.

Kumekuwa na mkaanganyiko wa kisiasa kati ya Wajumbe wa bunge na sherehe ndani bunge wakati mada ikiwa imetolewa na baadae kuendelea nayo.

Mazungumzo hayo yalitarajiwa kuanza saa 10 na nusu jioni leo hadi saa 3 asubuhi na kuunda Kamati ya wanachama 9.


Mchungaji wa Zanu PF, Cde Lovemore Matuke, alisema Rais Mugabe anatarajiwa kupata barua ya matokeo ya kesho jioni (Jumatano) au Alhamisi asubuhi.
MAKAMU wa rais wa zamani Emmerson Mnangagwa, ambaye alifutwa kazi na kusababisha jeshi kuchukua mamlaka ya nchi , amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja.

Amesema alitoroka nje ya nchi wiki mbili zilizopita wakati alipobaini kuwa kuna njama za kumuua na hatarejea nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wake huku Chama cha rais Mugabe kikijiandaa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuwa rais ajaye wa Zimbabwe

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.


Mugabe alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba na kuwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu  badala yake katika hotuba yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.
TUME ya uchaguzi imeahirisha uchaguzi katika kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay.
Vituo vya kura katika baadhi ya maeneo tayari vimefungwa.

Kinyume na uchaguzi wa mwezi Agosti, katika vituo vya kupigia kura hakukuwa na foleni ndefu.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesusia uchaguzi huo na kuwataka wafuasi wake wasalie manyumbani

Uchaguzi huu unatokana na hatua ya Mahakama ya Juu kufuta uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti

UCHAGUZI NI VURUGU KENYE



Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.
Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa.
Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana
Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.
Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo.

WAKUU wa mbalimbali wa kapuni za utengenejaji magari nchini Ujerumani wamekubaliana mapema wiki iliyopita katika mkutano wa kilele uliowakutanisha na viongozi wa kisiasa kutumia kiasi cha Euro Milioni 500, sawa na Dola Milioni 592 katika kuboresha programu za kompyuta katika magari milioni 5.3 yanayotumia nishati ya dizeli.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kurejesha imani kwenye sekta hiyo ilikuwa imechafuliwa.Huku kampuni za kutengeneza magari yalionekana kujiweka kando juu ya shinikizo la kisiasa lililotaka mabadiliko ya gharama kubwa zaidi za vifaa

Watengenezaji hao wa magari waliokutana mjini Berlin, Volkswagen, pamoja na chapa zake za kifahari Audi na Porsche, BMW, Daimer, Ford ya Ujerumani na chapa inayomilikiwa na kampuni ya Ufaransa, Opel, walikubalina kuboresha programu hizo kama sehemu ya hatua za mfululizo za kushughulikia mzozo unaovikabili viwanda vinavyotengeneza magari yanayotumia dizeli.

Barbara Hendricks ambaye ni Waziri wa Mazingira alisisitiza uboreshaji wa programu yalikuwa ni hatua ya awali kuelekea kuboresha viwango vya uchafuzi wa hali ya hewa hewa. Na kukiri mbele ya waandishi wa habari baada ya mkutano huo kwamba maazimio yaliyoazimiwa katika mkutano huo hayatajitosheleza.

Waziri Mkuu wa Jimbo la Kati la Lower Saxony, ambako ndiko makao ya kampuni ya magari ya Volkswagen, Stephan Weil yaliko alisema msukumo wa kuboreshwa kwa programu hizo utaendelea.
mwezi Septemba 2015, Sekta ya magari iliyumba wakati Volkswagen ilipokiri kufunga vifaa kwenye magari yake ambavyo vinatoa taarifa za uongo za vipimo vya nishati ya dizeli katika uchafuzi wa mazingira kwa zaidi ya magari milioni 11 duniani kote.
Mzozo huo uliongezeka baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu makampuni matano ya magari, Volkswagen, Audi, Porsche, BMW na Daimler, yalikuwa yameunda genge la siri la wafanyabiashara ambao miongoni mwa mambo mengine hujadiliana kuhusu viwango na namna ya kudhibiti utoaji wa gesi chafu tangu miaka ya 1990.
Utafiti wa maoni uliotolewa na taasisi ya YouGov siku za hivi karibuni ulionyesha kuwa ni asilimia 41 tu ya Wajerumani wenye imani ya sekta ya magari, ambayo inaajiri watu 828,000, inayowakilisha asilimia 14 ya nguvu kazi kwenye sekta ya uzalishaji nchini Ujerumani.

Mkutano huo pia uliunda sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa shirikisho la Ujerumani utakaofanyika Septemba 24, huku chama cha Kansela Angela Merkel cha CDU kikikosolewa kwa kuendeleza uhusiano uliopitiliza na watengenezaji wa magari na namna kilivyoshughulikia mzozo wa uchafuzi wa hali ya hewa.

Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na mawaziri wakuu wa majimbo matano ya Ujerumani ambako ndiko yaliko makao makuu ya kampuni ya magari hayo pia uliadimia kutoa kiasi cha Euro Milioni 500 kushughulikia matatizo ya uchafuzi wa mazingira ya mijini, na  kuanzisha mfuko wa ruzuku unayolenga kuboresha na kuendeleza mifumo ya usafi kwenye sekta ya usafiri.



- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -