WAKUU wa mbalimbali wa kapuni za utengenejaji magari nchini Ujerumani wamekubaliana mapema wiki iliyopita katika mkutano wa kilele uliowakut...
WAKUU wa mbalimbali wa kapuni za utengenejaji
magari nchini Ujerumani wamekubaliana mapema wiki iliyopita katika mkutano wa
kilele uliowakutanisha na viongozi wa kisiasa kutumia kiasi cha Euro Milioni
500, sawa na Dola Milioni 592 katika kuboresha programu za kompyuta katika
magari milioni 5.3 yanayotumia nishati ya dizeli.
Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kurejesha
imani kwenye sekta hiyo ilikuwa imechafuliwa.Huku kampuni za kutengeneza magari
yalionekana kujiweka kando juu ya shinikizo la kisiasa lililotaka mabadiliko ya
gharama kubwa zaidi za vifaa
Watengenezaji hao wa magari waliokutana mjini
Berlin, Volkswagen, pamoja na chapa zake za kifahari Audi na Porsche, BMW,
Daimer, Ford ya Ujerumani na chapa inayomilikiwa na kampuni ya Ufaransa, Opel,
walikubalina kuboresha programu hizo kama sehemu ya hatua za mfululizo za
kushughulikia mzozo unaovikabili viwanda vinavyotengeneza magari yanayotumia
dizeli.
Barbara Hendricks ambaye ni Waziri wa Mazingira
alisisitiza uboreshaji wa programu yalikuwa ni hatua ya awali kuelekea
kuboresha viwango vya uchafuzi wa hali ya hewa hewa. Na kukiri mbele ya
waandishi wa habari baada ya mkutano huo kwamba maazimio yaliyoazimiwa katika
mkutano huo hayatajitosheleza.
Waziri Mkuu wa Jimbo la Kati la Lower Saxony,
ambako ndiko makao ya kampuni ya magari ya Volkswagen, Stephan Weil yaliko alisema
msukumo wa kuboreshwa kwa programu hizo utaendelea.
mwezi Septemba 2015, Sekta ya magari iliyumba wakati
Volkswagen ilipokiri kufunga vifaa kwenye magari yake ambavyo vinatoa taarifa
za uongo za vipimo vya nishati ya dizeli katika uchafuzi wa mazingira kwa zaidi
ya magari milioni 11 duniani kote.
Mzozo huo uliongezeka baada ya vyombo vya habari
kuripoti kuhusu makampuni matano ya magari, Volkswagen, Audi, Porsche, BMW na
Daimler, yalikuwa yameunda genge la siri la wafanyabiashara ambao miongoni mwa
mambo mengine hujadiliana kuhusu viwango na namna ya kudhibiti utoaji wa gesi
chafu tangu miaka ya 1990.
Utafiti wa maoni uliotolewa na taasisi ya YouGov
siku za hivi karibuni ulionyesha kuwa ni asilimia 41 tu ya Wajerumani wenye
imani ya sekta ya magari, ambayo inaajiri watu 828,000, inayowakilisha asilimia
14 ya nguvu kazi kwenye sekta ya uzalishaji nchini Ujerumani.
Mkutano huo pia uliunda sehemu ya maandalizi ya
uchaguzi wa shirikisho la Ujerumani utakaofanyika Septemba 24, huku chama cha
Kansela Angela Merkel cha CDU kikikosolewa kwa kuendeleza uhusiano uliopitiliza
na watengenezaji wa magari na namna kilivyoshughulikia mzozo wa uchafuzi wa hali
ya hewa.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa
na mawaziri wakuu wa majimbo matano ya Ujerumani ambako ndiko yaliko makao
makuu ya kampuni ya magari hayo pia uliadimia kutoa kiasi cha Euro Milioni 500
kushughulikia matatizo ya uchafuzi wa mazingira ya mijini, na kuanzisha
mfuko wa ruzuku unayolenga kuboresha na kuendeleza mifumo ya usafi kwenye sekta
ya usafiri.
COMMENTS