Habari Mpya

Friday, 18 August 2017

ZAIDI ya Shilingi bilioni moja zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja la mto Mzinga, jimbo la Ukonga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 kupitia fedha za Manispaa na mfuko wa jimbo.


Ahadi hiyo ilitolewa na mbunge wa jimbo, Mwita Waitara wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakazi wa Kata za Msongola na Kitunda ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa na adha ya usafiri baada ya daraja hilo kuharibiwa na mafuriko.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -