Juma anakabiliwa na tatizo la kwenda haja kubwa kwa kutumia mipara kupitia tundu alilochanwa tumboni baada ya matibabu kuthibitisha kuwa m...
Juma anakabiliwa na tatizo la kwenda
haja kubwa kwa kutumia mipara kupitia tundu alilochanwa tumboni baada ya
matibabu kuthibitisha kuwa mfumo wake wa haja kubwa umekufa.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa kijana
huyo, Sofia Jackson anasema ameelezwa na matabibu kuwa hakuna namna nyingine ya
Juma kujisaidia haja kubwa isipokuwa kwa mipira katika maisha yake yote.
KUANZWA NA MATATIZO:
Juma
alizwaliwa mwaka 2001 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu.
Alianza shule ya msingi akiwa nia ya kuendelea hadi chuo kikuu. Alianzwa na
tatizo hilo alipofikisha umri wa miaka 15 Machi mwaka jana.
Juma
alipaswa kuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka huu katika shule ya TUT
anamosoma, lakini kutokana na hali yake hiyo alishindwa kufanya mtihani wa taifa
wa kidato cha pili mwaka jana.
Kwa
sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo lakini kutokana na hali hiyo
anashindwa kwenda shuleni kama inavyotakiwa. Ndoto yake ni kuendelea na masomo
hadi elimu ya juu.
“Natamani
kufikia ndoto yangu ya kuwa mwanataaluma kwa masomo yangu ya chuo kikuu. Lakini
tumaini langu limeingia moto. Sikujua ningekuwa katika hali hii, hata kwa sasa
naishindwa kukaa bweni na wezangu kwa hofu ya usumbufu kwa wenzangu, naomba kama
wapo watu wanaoweza kunisaidia wajitokeza kujaribu matibabu kwingine,”alisema
Juma.
HARAKATI ZA MATIBABU:
Kwa sasa anamtegemea mama yake kwa ada na matibabu baada ya baba
yake mzazi kufariki. Mama yake ni muuuza mbogamboga kwa mtaji mdogo sana ambao
hawezi kumudu kununua mipira , dawa na vifaa tiba vingine pamoja na kulipa ada,
anasema.
Baada ya kuona hali hiyo
isiyokuwa ya kawaida kwa mwanae, Sofia anasema alimpeleka mwanae
walianza hospitali yaMbezi
kisha
kushauriwa kumpeleka. hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.
“Pale
Mwananyama walishindwa, wakatupa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili,
walimfanyia upasuaji na kupata nafuu. Walifanyia vipimo vingine, na kubaini
kwamba hakuna namna yoyote ya kupata choo, isipokuwa kupitia tobo ambalo
ametobolewa tumboni ili ajisaidie kwa njia ya mpira,” alisema.
Mama
huyo analalamika kuwa tangu mumewe kufariki dunia amekuwa na mzigo mkubwa kumhudumia
Juma na wadogo zake, huku akiomba msaada kwa wasamaria kwa ajili ya kufanikisha
matibabu ya kijana wake nje ya nchi.
WITO:
Kijana
Daud Juma anaiomba serikali na wanajamii kwa ujumla, kumchangia pesa
zitakazofanikisha kutibiwa nchini India ambako ameshauriwa na baadhi ya
wataalamu.
Pia
ameiomba serikali kupunguza au kuondoa kabisa gharama za matibabu kwa watu
wenye matatizo makubwa yasiyotibika ndani ya nchi kwani watanzania wengi
wamejikuta wa kipoteza maisha kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Pia
ameomba wasamaria wema ikiwamo taasisi za serikali na binafsi kumsaidia mama
yake kuimarisha mtaji wake kutokana na mtaji wake wa sasa kuwa mdogo huku akiwa
na jukumu kubwa la kumlea yeye (Juma) na wadogo zake.
“Natamani
kurudi shuleni kuungana na wenzangu ili kutimiza ndoto zangu, lakini mama
amekwama na hatuna mtu wa kutusaidia.
Tumekuwa
watu wa kusaidiwa chakula na majirani. Katika hali hiyo, tutawezaje kupata pesa
za matibabu? alisema Juma
COMMENTS