Powered by Blogger.

About

[Michezo kimataifa][column2]

Labels

Blog Archive

Search This Blog

Blog Archive

[random][featured1]

BTemplates.com

MICHEZO KITAIFA

[michezo][column2]

Blogroll

[afya][fbig2]

Contact us

Name

Email *

Message *

BTemplates.com

UHAMIAJI KUREJESHA PASIPOTI ZENYE HADHI YA KIDIPLOMASIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI                                            IDARA YA UHAMIAJI       ...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                                           IDARA YA UHAMIAJI      


TAARIFA KWA UMMA

KUREJESHA PASIPOTI ZENYE HADHI YA KIDIPLOMASIA NA KIUTUMISHI KWA WASIOSTAHIKI
Idara ya Uhamiaji inapenda kuufahamisha Umma kwamba, utolewaji wa pasipoti zenye hadhi ya Kidiplomasia (Diplomatic Passport) na Kiutumishi (Service Passport) upo kwa mujibu wa Sheria ya Pasipoti na Hati za Kusafiria Sura ya 42 ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni zake.
Katika Vifungu Namba 10(2) na (3) na Jedwali la Pili na la Tatu la Sheria hiyo, makundi mbalimbali ya watu wanaostahiki kupewa pasipoti hizo yameainishwa.

Hivyo, Idara ya Uhamiaji inawataka wale wote ambao wamefikia ukomo wa Utumishi wa nyadhifa na hadhi hizo, warejeshe pasipoti hizo kwenye Ofisi za Uhamiaji ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii, kama yalivyo matakwa ya Kifungu cha 8(2) cha Sheria tajwa hapo juu; isipokuwa wale ambao kwa mujibu wa nyadhifa zao wanaruhusiwa kisheria kuendelea kutumia Pasipoti hizo hata baada ya kustaafu kwao wakiwemo Viongozi Wakuu wa Nchi wastaafu, Wakuu wa Mihimili ya dola Wastaafu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wastaafu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu kwenye Sheria hiyo.

Baada ya kuisha kwa kipindi tajwa yaani mwezi mmoja baada ya kutolewa kwa taarifa hii, wasiostahiki kuwa nazo watazuiliwa safari zao mara watakapopita katika vituo vya kuingia na kutoka nchini ikiwa ni pamoja na Viwanja vya Ndege. Aidha, ieleweke kwamba, kuendelea kuwa na Pasipoti hizo kwa wasiostahiki ni kosa kisheria chini ya kifungu cha 19(2)(k) cha Sheria tajwa.

Imetolewa na

KITENGO CHA UHUSIANO,
IDARA YA UHAMIAJI,
MAKAO MAKUU.

15 AGOSTI, 2017.

COMMENTS

[facebook]
Name

AFYA,6,GURUDUMU LA MAISHA,2,HABARI,48,KIJIJINI,7,KIMATAIFA,9,MAHUSIANO NA SAIKOLOJIA,2,MAKALA,2,MAKALA YA ELIMU,1,MICHEZO,2,MIKOANI,4,SARAFU,4,VIDEO,4,ZANZIBAR,1,
ltr
item
LENZI MEDIA: UHAMIAJI KUREJESHA PASIPOTI ZENYE HADHI YA KIDIPLOMASIA
UHAMIAJI KUREJESHA PASIPOTI ZENYE HADHI YA KIDIPLOMASIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEieRowanvlARuXormMhDwKhjj_2ihqeMWOxdeWkL6x5sm1cZz2q8cFdxw0oi6C8SfSZ-v3E4jJ4MmtlTa_9g30GbwH1gww6mkc8NZf_42Cx6iCWVV567DX-MXur00IL7hVIWYP8dt2h830/s640/uhamiaji.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEieRowanvlARuXormMhDwKhjj_2ihqeMWOxdeWkL6x5sm1cZz2q8cFdxw0oi6C8SfSZ-v3E4jJ4MmtlTa_9g30GbwH1gww6mkc8NZf_42Cx6iCWVV567DX-MXur00IL7hVIWYP8dt2h830/s72-c/uhamiaji.JPG
LENZI MEDIA
https://lenzimedia.blogspot.com/2017/08/jamhuriya-muungano-wa-tanzania-wizaraya.html
https://lenzimedia.blogspot.com/
https://lenzimedia.blogspot.com/
https://lenzimedia.blogspot.com/2017/08/jamhuriya-muungano-wa-tanzania-wizaraya.html
true
2372332392983471599
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content