KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kimesema kuwa mkoa minne ndani chini inaongoza kwa ukiukwaji wa ukiukwaji wa haki za wan...
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kimesema kuwa
mkoa minne ndani chini inaongoza kwa ukiukwaji wa ukiukwaji wa haki za wanawake
na watoto unaofanyika kupitia ukatili wa kijinsia, kingono, ulawiti, unajisi,
ukeketaji na unyanyapaa.
Mkurugenzi Mtendaji
wa LHRC, Hellen Kijo-Bisimba alisema matukio hayo yameshamiri katika mikoa ya
Tabora, Dar es Salaam, Mbeya na Iringa bado yameonekana kuendelea kuwa
tishio kwa ustawi wa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen Kijo-Bisimba akiongea na wandishi wa habari |
“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa tumegundua kwamba mikoa hiyo
bado inaongoza kwa ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto”
Bisimba alisema jeshi la polisi linapaswa kukomesha vitendo hivyo kubadilisha
mbinu za kiutafiti na upelelezi wa kesi mbalimbali ili kuhakikisha watuhumiwa
wanaopatikana wanachukuliwa sheria kali.
Ameongeza kwamba kipindi cha nusu mwaka hali ya haki
za binadamu nchini bado ni mbaya ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Haliyo imesababishwa na ukiukwaji wa haki za kiraia, kisiasa, haki
ya kuishi, kuminywa kwa haki na uhuru wa kujieleza pamoja na kuzuiwa kwa haki
ya kukusanyika.
COMMENTS