CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar kwa moyo mkunjufu kinapongeza na kuisifu kitendo kilichofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuon...
CHAMA Cha
Mapinduzi Zanzibar kwa moyo mkunjufu kinapongeza na kuisifu kitendo
kilichofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuongeza
pencheni kwa Wastaafu waliomaliza utumishi wao wakipokea mshahara wa
kima cha chini serikalini.
Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu. (PICHA YA MAKTABA YA AFISI KUU CCM-ZANZIBAR) |
Kwa mujibu
wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Waride Bakari Jabu amesema
ongezeko la shilingi 50,000 ni sawa na asilimia 125 lililofanywa na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, linajibu masuala mengi ya msingi ya kiuchumi,
kisiasa na kijamii.
Akielezea
kufarajika kwake na kiwango hicho cha pencheni kilichoongezwa kwa wastaafu,
Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar amesema suala la
kuongeza shilingi 50,000 hadi kufikia shilingi
90,000 kinatakiwa kupongezwa na wananchi.
Amesema
kitendo hicho kilikofikiwa na Serikali (SMZ) cha kuamua kuwaongezea wastaafu
wake pensheni kinalenga sio tu kuwasaidia wastaafu hao kupambana na hali
ngumu ya maisha, bali pia kwa kiasi kikubwa kitaleta uwiyano wa karibu na
nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wa Serikali liyofanyika hivi karibuni.
Ameeleza kuwa CCM pia inaipongeza serikali ya
awamu ya saba kwa imeimarisha maslahi ya watumishi wa umma katika kuongeza
viwango vya mishahara ya kima cha chini kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi
300,000 ambalo ni ongezeko la asilimia 100, pamoja na kutekeleza mpango wa utoaji wa pencheni jamii kwa wazee
wote waliofikisha miaka 70 bila ya kujali kazi aliyokuwa akiifanya.
Hata
hivyo, Waride ameiomba Serikali kupitia Wizara yenye Mamlaka ya Fedha kufanya
kila linalowezekana kuhakikisha wastaafu waliokuwa na nyadhifa serikalini
wanapatiwa pensheni kulingana na nyadhifa walizokuwa nazo hapo kabla.
Pia amesema CCM inaridhishwa na kasi ya Dkt. Shein katika Utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015/2020, hivyo tunawasihi wananchi na
viongozi wa Serikali kufuata nyayo hizo kwa kumsadia kiongozi huyo ili Taifa
lizidi kuimarika kiuchumi.
COMMENTS