BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga limewafukuza kazi wakuu wa idara nguli wawili kutokana na mak...
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Ushetu Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga limewafukuza kazi wakuu wa idara nguli wawili kutokana
na makosa mbali mbali ikiwemo matumizi mabaya ya Madaraka na mali ya umma.
Akitoa maamuzi ya kufukuzwa kwa watumishi hao
muda Mfupi baada ya baraza la madiwani kujigeuza kuwa kamati ili kupata fursa
ya kujadili ripoti ya uchuguzi dhidi ya watumishi hao ,Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Juma Kimisha alisema kuwa baraza limejiridhisha pasipo
shaka na kuweza kuwatia hatiani.
Kimisha aliwataja watumishi hao kuwa ni pamoja
na Afisa kutoka idara ya Mipango na ufuatiliaji na Takwimu Fredrick
Mallya ambaye alikuwa na makosa manne ambapo kati ya hayo ni moja tuu ambalo
hakupatikana na hatia.
Alisema kuwa kamati imechunguza na kubaini kuwa
hakukutwa na hatia moja ya kuratibu taarifa ya Mkoa na kusababisha
mkurugenzi wake kufukuzwa katika kikao cha kuwasilisha bajeti ya mkoa mzima.
Alisema kuwa kosa la pili la mtumishi huyo ni
kupatikana na hatia ya kutotii wito wa katibu Tawala wa Mkoa na kosa la
tau ni kutotii maagizo mbalimbali ya mkurugenzi anapomwagiza huku kosa la Nne
ni kushindwa kuwasilisha bajeti ya halmashauri ya wilaya kwenye
majumuisho ya bajeti Dar es salaam na badala yake alikaa siku 4 kati ya siku 19
alizotakiwa kukaa huko.
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo alisema kuwa kati
ya makosa hayo, kosa la kwanza la kushindwa kuratibu taarifa ya mkoa ndilo kosa
ambalo hakutiwa hatiani lakini makosa mengine amekutwa na hatia.
Mtumishi mwingine ni Mkuu wa idara ya fedha na
Biashara Stephen Nyeriga, baada ya kamati kuchunguza imebaini kuwa
mtumishi huyo alikuwa na makosa sita na kati ya hayo makosa matano
amekutwa na hatia.
Alisema kuwa makosa hayo ni pamoja na kutotii wito wa
katibu tawala wa Mkoa , kosa la pili ni kushindwa kusimamia mapato ya
halmashauri na kusababisha baadhi ya vitabu kupotea na kuingia kwenye mikono ya
wajanja, na kosa la tatu nikusababisha migongano kati ya ofisi ya Mkurugenzi na
watumishi.
Makosa mengine ni pamoja na kushindwa kuandaa Maduhuli
ya Halmashauri kwa ajili ya lipoti mbalimbali, na kosa la tano ni kushindwa
kutekeleza maagizo ya Mkurugenzi wake huku kosa la sita likiwa ni kushindwa
kuwasilisha bajeti ya halmashauri Ngazi ya Taifa hali ambayo imechangia
Halmashauri kupata hati yenye mashaka.
Kutokana na hali hiyo Baraza hilo limeridhia kwa kauli
moja na kwamba kufukuzwa kwa watumishi hao kutaongeza nidhamu katika utumishi
wa umma kwenye halimashauri hiyo ikiwa nipamoja na mishingi ya kazi
iliyowekwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Michael
Matomora aliwataka watumishi wengine waliosalia kuhakikisha wanakuwa na
uadilifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani hali hiyo inachangia
kushindwa kuwatumikia wananchi.
Alisema kuwa watumishi waliopo wanatakiwa kufanya kazi
kwa uadilifu na kumuunga mkono raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kukabiliana na ubadhilifu wa
fedha za umma na kwamba kufanya hivyo kutaleta heshima kwa Mtumishi Mwenyewe na
halmashauri.
COMMENTS