Habari Mpya

Wednesday, 16 August 2017

WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa, ameondoka nchini leo (Jumatano, Agosti 16, 2017) kuelekea nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolew na ofisi ya Waziri mkuu kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam, ziara hiyo nchini Cuba Majaliwa anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za afya, elimu utalii na Kilimo.
Cuba ni miongoni mwa nchi zenye uhusiano mzuri na Tanzania kwa mrefu Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.
Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes alifanya ziara na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kuendeleza, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji. Nchi nyingine ambazo Valdes alitembelea siku hiyo ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo- DRC, Botwana na Zimbabwe. 


Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -