RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja kutangaza na kuelim...
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka Uongozi wa Mkoa
wa Kusini Unguja kutangaza na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuenzi dhana ya
Utalii wa ndani.
Kauli hiyo aliitoa katika majumuisho ya ziara ya Mkoa huo
iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), alisema dhana
ya utalii wa ndani ni muhimu kuendelea kutangawa kwani imebeba fursa
zitakazoongeza pato la taifa kupitia sekta ya utalii nchini.
Dk. Shein alipongeza hatua
za maendeleo zilizofikiwa na Mkoa huo katika sekta za kilimo, utalii, afya, miundombinu
na hatua zilizowekwa za kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi.
Kupitia majumuisho
hayo Dk. Shein aliwaagiza
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga utamaduni wa kutembea vijijini kwa lengo la kuwaelimisha
wananchi juu ya fursa zinazopatikana katika wizara hizo ili wananchi wazifahamu na kuzichangamkia.
“ Bado kuna wananchi hawajui kama serikali ina mfumo wa
uwezeshaji unatoa mikopo kwa
wajasiriamali na vikundi vingine vyenye malengo ya kujikomboa kiuchumi, na hadi
hivi sasa tayari zaidi ya bilioni mbili wamekopeshwa wananchi wa maeneo mbali
mbali hapa nchini”, alieleza Dk. Shein na kuitaka Wizara ya kazi, Uwezeshaji,
Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar
kutangaza kuwafikia wananchi wa vijijini ili wanufaike na mfuko huo.
Dk. Shein aliwapongeza wakulima wa zao la ndimu ndani ya
mkoa huo na kuitaka Wizara inayohusika
na masuala ya kilimo kutumia wataalamu wake
kuwafundishe wananchi mbinu bora za kilimo cha kisasa.
Hata hivyo alisema licha ya Mkoa huo kupata mafanikio mbali
mbali bado wanatakiwa kuzidisha bidii katika kudhibiti vitendo vya magendo ya
bidhaa mbali mbali vinavyoikosesha serikali mapato.
Dk. Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar alizindua jengo la Tawi la CCM
Kizimkazi Dimbani ndani ya Mkoa huo, na
kuwasihi viongozi wa chama hicho kutumia vikao vya kikatiba wakati wa kufanya
maamuzi yanayohusu taasisi hiyo badala
ya kufanya maamuzi binafsi.
Aliwasihi wazee wa CCM kuendeleza utamaduni wa kuwafundisha itikadi
vijana ili waweze kujua historia ya chama na nchi ilipotoka kabla na baada ya
mapinduzi ya mwaka 1964.
Aliwambia
wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuwa Chama cha
Mapinduzi kinapoahidi kinatekeleza kwa wakati kwani miradi yote
inayozinduliwa hivi sasa imetokana na usimamizi mzuri wa Ilani ya
uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2016.
Ziara hiyo ya siku mbili katika Mkoa wa Kusini, Dkt. Shein
alikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu katika
kijiji cha Kitogani, alitembelea wajasiriamali wa Saccos ya AMCO na kuona mazao
wanayozalisha yakiwemo Matikiti maji, mihogo, ndimu na Tungule huko Mtule
kijiji cha Paje.
Miradi mingine iliyotembelewa na Dk. Shein ni kukagua mradi
wa kisima cha maji safi na salama huko katika mapango ya Mnywambiji pamoja na
kuweka jiwe la msingi katika nyumba za kuishi za madaktari wa Vituo vya Afya
vya Kajengwa na Muyuni ‘B’ Wilaya ya
Kusini Unguja.
COMMENTS