Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amekabidhi mabati zaidii ya 400 kwa ajili ya kukamilsha ujenzi wa shule za msingi na sekondari,vituo vy...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amekabidhi mabati zaidii ya 400 kwa ajili ya kukamilsha ujenzi wa shule za msingi na sekondari,vituo vya afya pamoja na zahanati katika Halmashauri ya Meru ambayo aliahidi wakati wa ziara ya yake wilayani Arumeru mwishoni mwa mwezi Julai.
Gambo akizungumza mara baada yakukabidhi mabati hayo ambayo yametolewa na kampuni ya China ya ujenzi wa barabara ya Arusha Tengeru,Hanil Jiangsu Joint Venture LTD -amesema hatua hiyo ya kutoa msaada wa mabati ni kuwatia moyo wananchi ili waweze kuchangia shuguli za maenedeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo |
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri Happyness Mrisho ameahidi kutumia mabati hayo kama ilivyokusudiwa katika kutekeleza ujenzi wa shule,vituo vya afya na zahanati.
COMMENTS