Bodi ya Pamba Tanzania wilayani Maswa mkoani Simiyu imefanya operesheni maalumu ya kuwakagua wanunuzi na wauzaji wa Pamba ambao wamekuwa wa...
Bodi ya Pamba Tanzania
wilayani Maswa mkoani Simiyu imefanya operesheni maalumu ya kuwakagua wanunuzi
na wauzaji wa Pamba ambao wamekuwa wakichafua zao hilo kwa kuichanganya
mchanga, maji na udongo ili kuongeza uzito na kupata faida mara mbili ambapo
katika huku oporesheni wakulima na wanunuzi wamepongeza zoezi hilo linaloondoa
udanganyifu katika zao hilo.
Wakiongea katika
ukaguzi huo baadhi ya wanunuzi na wakulima katika vijiji vya Mwabayanda na
Nguliguli walisema kuwa zoezi hilo ni zuri kwa sababu linawafanya wajitathini
na kufahamu ubora wa pamba wanayoinunua pia kuwakumbusha wakulima kutoharibu
pamba yao.
Kampuni ya Kahama Cotton Co Ltd ya mjini Kahama mkoani Shinyanga |
‘’zoezi hili tunaomba
liwe endelevu kwa sababu linagusa wakulima na wanunuzi kuwa yoyote atakayekutwa
na kosa anahukumiwa hapohapo, litaondoa uchafuzi wa pamba na kuongeza ubora
wake hivyo litakuza soko la pamba kimataifa ambayo awali ilikuwa imeshuka
kutokana na pamba yetu kuwa chafu’’ alisema Nkuba Minoja.
John Ng’hona alisema
kuwa pamoja na ukaguzi huo, katika msimu ujao watuletee mbegu ya pamba na
pembejeo kwa wakati ili tuweze kulima kwa uhakika na kuongeza uzalishaji.
‘’tulikuwa tukiletewa
mbegu zisizoota hapo awali, dawa isiyouwa wadudu…hivyo tunaomba wazingatie haya
ili wakulima waweze kuona thamani ya zao hili pia tuongezewe maafisa ugani ili
waweze kuwafikia wakulima kuwashauri kulima kitaalamu’’ alisema Mtemi Ndahya.
Naye Mkaguzi wa Bodi ya Pamba wilayani humo Ally Maborouk alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na wanunuzi wanaoharibu pamba ni bora watafute biashara nyingine kwa kuwa bodi hiyo inasimamia wauazaji na wanunuzi na kuhakikisha pamba inayozalishwa na kuuzwa ni safi.
‘’wanunuzi wanaoharibu pamba ni bora watafute biashara nyingine, tutahakikisha pamba yote inayozalishwa na kuuzwa ni safi ili isiharibu soko la zao hilo kimataifa, tuko imara tutahakikisha tunawashughilikia ipasavyo’’ alisema Maborouk.
Aidha katika zoezi hilo lilioambata na mahakama inayotembea (mobile court) imekagua vituo vya pamba katika vijiji vya Nguliguli, Mwabayanda, Ilimbambasa, Senani, Zebeya na Mwabadimi na kuibua hoja baada ya mnunuzi mmoja wa pamba kampuni ya Gaki kijiji cha Igumangobo kufunga kituo na kuwakimbia wakaguzi hao.
Baada ya kuona hali
hiyo Mkaguzi wa Pamba aikifunga kituo hicho na kumwagiza mtendaji wa kijiji
kumkamata mnunuzi huyo ili aweze kueleza sababa zilizomfanya akikimbie kituo
chake.
Katika kijiji hichohicho cha
Igumangobo wanunuzi wawili Malugu Sungwandeba na George Salum wanunuizi wa
pamba Kampuni ya Kahama Cotton Co Ltd ya mjini Kahama mkoani Shinyanga
walipatikana na hatia baada ya kukiri kukutwa wamenunua pamba chafu
katika ghala lao
Katika mahakama hiyo inayotembea
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyalikungu,Lilian Kinyemi aliwahukumu washitakiwa
hao adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela kila mmoja au kulipa faini ya Sh
50,000 na Kampuni hiyo kuilipa bodi ya Pamba Sh 500,000 na washitakiwa walilipa
faini zote na kuachiwa huru.
COMMENTS