MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,amelishukuru Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) kwa kukamilisha mradi wa Barabara na...
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
,amelishukuru Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) kwa kukamilisha mradi wa
Barabara na bustani ya Kaburi moja iliyopo mtaa wa Samora jijini hapa.
Meya wa Jiji la Dar es SalaamIsaya Mwita akiteta jambo na mwakilishi wa JICA Nchini Tanzania Toshio Nagase |
Utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Desemba mwaka jana na
kusainiwa na meya huyo na baadae kukabidhiwa kwa halmashauri ya manispaa ya
Ilala leo.
Mwita alisema kuwa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi
milioni 840 ikiwa na malengo ya kuboresha mtaa wa samora ili kuwezesha magari
kutembea kwa uangalifu zaidi sambamba na kuliweka jiji kwenye muonekano mzuri.
Alisisitiza kuwa mradi huo uliochukua nafasi kubwa ya
maeneo ya maegesho ya magari, lakini umesababisha kuwa na muonekano mzuri
kutokana na maboresho yaliyofanyika.
Wakati huo huo mwakilishi wa JICA Nchini Tanzania Toshio
Nagase alieleza kuwa mradi huo utasaidia kupunguza msongamano wa magari katika
jiji la Dar es Salaam.
COMMENTS