- Home >
- Msemaji wa jeshi ncini Kenya aliyedaiwa kutoweka ajitokeza
Tuesday, 1 August 2017
Wizara ya ulinzi nchini Kenya imeshutumu taarifa zilizokuwa zimeenezwa kwamba msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Joseph Owuoth alikuwa ametoweka.
"Kanali J. M. Owuoth hajatoweka na yuko nasi hapa, akiwa hai na mzima wa afya," alisema Bi Omamo.
Kanali huyo alikuwa ameandamana na waziri kwenye kikao hicho.
![]() |
Kanali Owuoth (kulia) aliandamana na Waziri Omamo wakati wa kikao na wanahabari |
Kanali Owuoth aligonga vichwa vya haKIMATAIFAbari baada ya kuthibitisha kwamba nyaraka zilizokuwa zimetumiwa na muungano wa upinzani nchini humo Nasa kudai kwamba serikali inapanga kutumia jeshi kutekeleza 'mapinduzi' ili kuendelea kusalia madarakani zilikuwa halisi.
Msemaji huyo hata hivyo alisema nyaraka hizo zilinukuliwa na kufasiriwa visivyo.
Bi Omamo, kwenye kikao hicho, alisema baada ya uchunguzi, imebainika kwamba nyaraka hizo zilizotumiwa na muungano wa Nasa zilikuwa ghushi.
Taarifa za kudaiwa kutoweka kwa Kanali Owuoth zilikuwa zimezua wasiwasi mkubwa kwani zilijiri siku moja baada ya mwili wa meneja wa teknolojia katika Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Chris Msando, aliyetoweka Ijumaa usiku, kupatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City jijini Nairobi pamoja na mwili wa mwanamke mwingine.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati aliambia wanahabari kwamba hakukuwa na shaka kwamba Bw Msando aliteswa kabla ya kuuawa na kuwataka polisi wafanye uchunguzi wa kina kufumbua kitendawili kuhusu kuuawa kwake.