Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wametakiwa kuongeza jitahada za kuwasajili wanachama wengi wa mfuko huo ili vituo vya serikali viweze...
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
wametakiwa kuongeza jitahada za kuwasajili wanachama wengi wa mfuko huo ili
vituo vya serikali viweze kutoa huduma kwa wananchi wengi
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na
Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ummy mwalimu wakati
alipotembelea kituo cha afya cha Mazwi kilichopo katika Manispaa ya Wilaya ya
Sumbawanga mwishoni.
Alisema Mkoa wa Rukwa umefikia asilimia
27 ya wananchi wanaotumia bima ya afya Kitaifa,hivyo waongeze kuwashawishi
wananchi wengi zaidi kujiunga na mfuko huo pamoja na mfuko wa afya ya
jamii(CHF)
“nimesema kuanzia sasa ninaanza kuwapima
kwa kusajili wananchi ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira,ninataka vijana
wengi wajiunge kwa wingi kwa kwa kujiunga kama kikundi na kujiunga na bima
inayojulikana kama ‘Kikoa” kwa kujiunga
kikundi cha kuanzia watu kumi,wafikieni huko huko walipo
Kwa upande wa Mfuko wa Afya ya
jamii(CHF) waziri huyo hivi sasa kuna CHF iliyoboreshwa hivyo kadi hiyo
inatumika kwenye vituo vyote vya halmashauri na si pale mwanachama alipokatia,”ni bora
tuwachangishe elfu kumi kumi za watanzania ili tuweze kufikia usajili wananchi
wengi na kupata huduma za afya bila vikwazo
Hata hivyo alishauri Manispaa hiyo
kutengezea kadi ambayo itakua rafiki kwa mwanachama kuweza kuiweka kwenye
waleti au mahali pengine ambayo itakua rahisi kwa kutunza na siyo kadi za hivi
sasa ambayo ni mzigo kwa mwanachama kuibeba kwani kadi hiyo ni kubwa
Pia, alisema wizara yake inataka
kuongeza gharama ya CHF iliyoboreshwa ya shilingi elfu ishirini ambapo mwenye kadi hiyo
ataenda kupata huduma hivyo hadi
hospitali ya mkoa,
“ tunazungumzia kila mtu apate huduma za
tiba bila kikwazo,leo una hela,kesho huna na una umwa bora tunasema utoe elfu
kumi na utibiwe ndani nya manispaa tena siyo peke yako bali na watu wako
watano,alisema waziri ummy.
Hata hivyo alisema ni marufuku
kwa mtu mwenye kadi ya CHF anapoenda kwenye vituo vya huduma ya afya
kuambiwa akanunue kipimo au dawa bali wanatakiwa kupata vipimo vyote.
COMMENTS