WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Balozi Benedict Mashiba, na ku...
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Balozi Benedict Mashiba, na
kumtaka kuimarisha mahusiano kati ya nchi zote mbili.
Akiongea na balozi huyo akiwa nyumbani kwake Oystabay leo jijini
Dar es Salaam, ambapo amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli zote
za Kidiplomasia kati ya Tanzania na
Malawi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii vilivyopo
nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na fursa za
uwekezaji zilizopo nchini hususan katika sekta ya viwanda.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa, (kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini MalawiBenedict Mashiba |
Majaliwa amesema licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio
vya utalii pia amemwambia juu ya kuboresha biashara kwa kutumia meli mbili za
mizigo za Mv. Ruvuma na Mv. Njombe alizozizindua hivi karibuni.
Amesema kuwa afanye mazungumzo na Watanzania waishio nchini Malawi
na kuwasisiza kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi husikaikiwa ni pamoja na kuwaunganisha
pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Balozi Mashiba amesema atahakikisha anayafanyia
kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama
pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Malawi.
COMMENTS