Habari Mpya

Saturday, 5 August 2017

Kama unataka kumshuhudia nyota Haruna Niyonzima akiwa Simba kwa mara ya kwanza usikosea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo.
Simbai arajia kuwasili Dar es Salaam leo Jumamosi na ndege ya Shirika la Rwanda wakitokea Afrika Kusini, walikokuwa kambini kwa takribani wiki tatu.
Kabla ya kufika Dar es Salaam, ndege hiyo itatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Remera, Rwanda na kumchukua Niyonzima kwa ajili ya maandalizi mengine.
Niyonzima ambaye anaheshimika kwenye soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na hasa Tanzania kutokana na uwezo wake alipokuwa anaichezea Yanga kwa takribani misimu mitano.
Alishindwa kushiriki kambi ya Simba nchini Afrika Kusini baada ya kupata matatizo ya visa.
Awali, bosi wa Simba, Zakaria Hans Poppe alisema: "Niyonzima atawepo Simba Day pamoja na Gyan (Nicolaus) wao wamechelewa kujiunga na wenzao kutokana na matatizo mbalimbali"

Gyan tayari amemalizana na Simba, kinachomchelewesha kujiunga na wenzake ni mkataba wake na Waghana unaisha Agosti 20.
Hivyo ametumiwa tiketi ya kuja Dar es Salaam kwenye Simba Day, atatambulishwa na baada ya hapo atarudi tena Ghana kwa ajili ya kumaliza mkataba wake na kuweka sawa mambo mengine.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -