WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao. ...
WAZIRI mkuu Kassim
Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao
pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao.
Mji wa Cuba |
Ametoa kauli hiyo jana
jioni (Jumapili, Agosti 20, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa Kitanzania
wanaosomea udaktari nchini Cuba.
Majaliwa ambaye yuko
nchini Cuba kwa ajili ya
ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Alisema uzalendo kwa Taifa ni jambo muhimu kwa sababu ya kukosa fursa nyingi za
kimaendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Kutokana na hali hiyo
Serikali inawasisitiza Wananchi kuwa wazalendo na washirikiane kuhakikisha
fursa za kimaendeleo zilizoko nchini zinaendelezwa.
Alisema Serikali
inatekeleza miradi mingi kwa lengo la kukuza uchumi kutoka chini kwenda wa
katikupitia ushirikiano.
Pia Waziri Mkuu
alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao kuzingatia sheria za nchini waliyoko
pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo yao.
Alisema Serikali
inatambua uwepo wao wa kimasomo nchini Cuba na kwamba inatarajia kupata mchango
mkubwa kutoka kwao punde wamalizapo masomo yao.
“Nawaomba msome
kwa bidii na mfaulu mitihani yenu. Elimu yenu iwasaidie katika ajira na muweze
kurejesha mikopo mliyopewa na Serikali ili iwanufaishe wengine.”
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu aliwataka Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa
mbalimbali kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii.
Alisema Tanzania
imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, hivyo ni vema Mabalozi
wakavitangaza jambo ambalo litasaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja
nchini.
Miongoni mwa vivutio
vya utalii vilivyoko nchini ni pamoja na mlima Kilimanjaro, visiwa vya
Zanzibar, mbuga mbalimbali zenye wanyama wa aina tofauti tofauti.
Awali Mwenyekiti wa wanafunzi hao, Goodchance
Tarimo alimuhakikishia Waziri
Mkuu kwamba watarejea nyumbani mara baada ya kumaliza masomo yao nchini humo.
Alisema wao wana imani kubwa na Serikali na
wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na viongozi wa Taifa kwa lengo la
kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi.
“Tunapongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya
Tano katika kujenga uchumi wa viwanda, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi
na ujenzi wa miundombinu ya kisasa”
COMMENTS