WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa mkoani Tabora kuacha kuwatumia watoto kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku bali wawapele...
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa mkoani
Tabora kuacha kuwatumia watoto kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku bali
wawapeleke shule.
Alitoa agizo hilo Jumapili, Agosti
13, 2017 alipokuwa annazungumza na watumishi idara za kilimo na ushirika na
viongozi wa wilaya ya mkoa huo kwenye kikao alichokiitisha ili kwa ajili ya
kuwapa maagizo.
Waziri mkuu Kasim Majaliwa akisisitiza jambo wakati anaongea na viongozi wa mkoa wa Tabora |
“Ninasisitiza jamii iwapeleke watoto shule kuanzia elimu ya awali hadi sekondari na tuache kuwatumia watoto wadogo kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. Wakuu wa wilaya simamieni eneo hili la kuondoa watoto kwenye ajira,” alisema.
Wakati huo
huo Majaliwa aliwataka viongozi hao kusimamia
elimu ya mtoto wa kike na kuhakikisha kuwa wanawalinda kuazia elimu ya msingi na
sekondari hatimaye wanapofikia ngazi ya chuo kikuu watakuwa wamepevuka na na
kujilinda wenewe.
Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya siku nne, aliwaasa vijana wa kiume wasithubutu kuwaoa mabinti wanaosoma, kwani kwa kufanya hivyo, wataishia kufungwa jela miaka 30.
Waziri mkuu akiongea na viongozi wa mkoa wa Tabora |
Katika ziara hiyo aliwaonya wazazi
wanaoamua kuwaoza mabinti zao ili wapate mahari, na na kuongeza kuwa kwa
kufanya hivyo wako katika hatari ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 endapo
watabainika kushirikiana na waoaji.
COMMENTS