Habari Mpya

Habari Zote

Showing posts with label MAKALA. Show all posts

TAHARIRI:


HAKUNA mashaka kwamba sasa tatizo la mafuriko sio kadhia kwa `watu  wa mabondeni’ au wanaoishi karibu na mkondo wa maji pekee.

Hata hivyo, nguvu kubwa imekuwa ikiwekwa katika  kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo hayo bila kutafuta na kuthibiti chanzo cha mafuriko hayo.

Mathalani,  katika jiji la Dar es Salaam, tumekuwa tukishuhudia wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi, Mkwajuni, Jangwani na kwingineko  jijini humo wakihamishwa, baadhi nyumba zao kuvunjwa.

Oktoba 26 mwaka huu, ilinyesha mvua kubwa nchini  na kusababisha madhara makubwa hasa jijini  Dar es Salaam, kwa mafuriko ya mvua hizo kuua watu  kadhaa, kuharibu mali zenye thamani kubwa.

Kila mtu atakuwa shahidi kupitia vyombo vya habari kuwapo kwa malalamiko ya athari za mafuriko hayo kila kona ya  jiji na maeneo mengine nchini.

Kama tulivyosema nguvu kubwa huelekezwa kwenye kuhamisha watu, hakuna  juhudi za kukabiliana na chanzo cha mafuriko. Ni kuokoa au kuhamisha tu.

Sisi tunaikumbusha serikali wajibu wake wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya majanga kwa kutambua kwamba chanzo cha mafuriko ni ongezeko la maendeleo ya watu
(Human Development Expansion) tunayoyataka!

Yapo maendeleo ya ongezeko la nyumba, shughuli za kibinadamu  kama vile kilimo, biashara na viwanda ambazo watalaamu wanasema vimekuwa chanzo cha ongezeko la mafuriko na kina cha maji ya bahari.

Kwa hiyo matatizo kama mmomonyoko wa udongo unaotokana na maji mengi yasiyovunwa kwenye nyumba, kukosekana kwa vizuia kasi  ya maji kama vile miti kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hujitokeza.

Matokeo yake ni kupanuka kwa makorongo, mito, bahari na maziwa  kila uchao na kupatikana kwa mabonde.

Bila kutambua wajibu wake katika kukabiliana na hali hiyo, serikali hukimbilia kuwaondoa watu kwa kigezo cha kisheria kwa kuwaita wavamizi wa  mita 60 za mito, bahari na maziwa  tena wengine sheria ya mazingira ya (EMA) ya mwaka 2004 iliwakuta.
Sisi tunaona kwamba kuna kila sababu ya serikali kutafuta chanzo cha mafuriko na kukithibiti. Hii ni pamoja na kujenga kingo za mito, bahari na maziwa ili kutopanuka na kufuata makazi ya watu.
Huu ni wajibu kulingana na mikataba ya kimataifa ambayo serikali yetu ilisaini na ni haki ya wananchi wa nchi husika.

Tunapokimbilia kuwahamisha watu wakati mabonde yalitokea kwa kutojengwa kingo, ni wazi kwamba hata wale ambao leo wako nje mita 60 kesho watakosa uhalali wa kuishi humo kutokana na mmomonyoko unaoendelea kuwafuata. Tutawahamisha wangapi? mwisho tutahamisha mtaa mzima!

Pia tunaishauri serikali kuimarisha miundombinu kwa kujenga au kufufua mitaro kutokana na ukosefu wa mitaro kusababisha kuzagaa kwa maji na kuwa chanzo kwa  watu wengine ambao sio wa mabondeni nao kuingia katika kadhia hiyo.

Sisi tunaamini kwamba hayo yakitiliwa mkazo tutapunguza au kumaliza tatizo la mara kwa mara la mafuriko. Haina maana kwamba waliojenga baada ya sheria waachwe. Msisitizo wetu ni jamii kutii sheria sambamba na kuthibiti chanzo cha tatizo kama haki ya jamii.

Kuwahamisha watu sio suluhisho na kukomesha tatizo. Ni sawa na kugawa vyandarua badala ya kuua mazalia ya mbu!
Juma anakabiliwa na tatizo la kwenda haja kubwa kwa kutumia mipara kupitia tundu alilochanwa tumboni baada ya matibabu kuthibitisha kuwa mfumo wake wa haja kubwa umekufa.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa kijana huyo, Sofia Jackson anasema ameelezwa na matabibu kuwa hakuna namna nyingine ya Juma kujisaidia haja kubwa isipokuwa kwa mipira katika maisha yake yote.

Mama huyo anasema Juma alianzwa na tatizo katika mazingira ya kutatanisha na baada ya kumpeleka katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu alipewa majibu hayo, huku nje ya hospitali akielezwa kuwa mtoto wake anaweza kufanyiwa upasuaji na kurudi kwenye hali yake ya kawaida ikiwa atampeleka Apolo nchini India.

KUANZWA NA MATATIZO:
Juma alizwaliwa mwaka 2001 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu. Alianza shule ya msingi akiwa nia ya kuendelea hadi chuo kikuu. Alianzwa na tatizo hilo alipofikisha umri wa miaka 15 Machi mwaka jana.


Juma alipaswa kuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka huu katika shule ya TUT anamosoma, lakini kutokana na hali yake hiyo alishindwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili mwaka jana.

Kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili shuleni hapo lakini kutokana na hali hiyo anashindwa kwenda shuleni kama inavyotakiwa. Ndoto yake ni kuendelea na masomo hadi elimu ya juu.

“Natamani kufikia ndoto yangu ya kuwa mwanataaluma kwa masomo yangu ya chuo kikuu. Lakini tumaini langu limeingia moto. Sikujua ningekuwa katika hali hii, hata kwa sasa naishindwa kukaa bweni na wezangu kwa hofu ya usumbufu kwa wenzangu, naomba kama wapo watu wanaoweza kunisaidia wajitokeza kujaribu matibabu kwingine,”alisema Juma.


HARAKATI ZA MATIBABU:
Kwa sasa anamtegemea mama yake kwa ada na matibabu baada ya baba yake mzazi kufariki. Mama yake ni muuuza mbogamboga kwa mtaji mdogo sana ambao hawezi kumudu kununua mipira , dawa na vifaa tiba vingine pamoja na kulipa ada, anasema.

 Baada ya kuona hali hiyo isiyokuwa ya kawaida kwa mwanae, Sofia anasema alimpeleka mwanae walianza hospitali yaMbezi
kisha kushauriwa kumpeleka. hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.

“Pale Mwananyama walishindwa, wakatupa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili, walimfanyia upasuaji na kupata nafuu. Walifanyia vipimo vingine, na kubaini kwamba hakuna namna yoyote ya kupata choo, isipokuwa kupitia tobo ambalo ametobolewa tumboni ili ajisaidie kwa njia ya mpira,” alisema.

Mama huyo analalamika kuwa tangu mumewe kufariki dunia amekuwa na mzigo mkubwa kumhudumia Juma na wadogo zake, huku akiomba msaada kwa wasamaria kwa ajili ya kufanikisha matibabu ya kijana wake nje ya nchi.

WITO:
Kijana Daud Juma anaiomba serikali na wanajamii kwa ujumla, kumchangia pesa zitakazofanikisha kutibiwa nchini India ambako ameshauriwa na baadhi ya wataalamu.

Pia ameiomba serikali kupunguza au kuondoa kabisa gharama za matibabu kwa watu wenye matatizo makubwa yasiyotibika ndani ya nchi kwani watanzania wengi wamejikuta wa kipoteza maisha kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Pia ameomba wasamaria wema ikiwamo taasisi za serikali na binafsi kumsaidia mama yake kuimarisha mtaji wake kutokana na mtaji wake wa sasa kuwa mdogo huku akiwa na jukumu kubwa la kumlea yeye (Juma) na wadogo zake.

“Natamani kurudi shuleni kuungana na wenzangu ili kutimiza ndoto zangu, lakini mama amekwama na hatuna mtu wa kutusaidia.


Tumekuwa watu wa kusaidiwa chakula na majirani. Katika hali hiyo, tutawezaje kupata pesa za matibabu? alisema Juma

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -