Habari Mpya

Tuesday, 21 November 2017

MAKAMU wa rais wa zamani Emmerson Mnangagwa, ambaye alifutwa kazi na kusababisha jeshi kuchukua mamlaka ya nchi , amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja.

Amesema alitoroka nje ya nchi wiki mbili zilizopita wakati alipobaini kuwa kuna njama za kumuua na hatarejea nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wake huku Chama cha rais Mugabe kikijiandaa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuwa rais ajaye wa Zimbabwe

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.


Mugabe alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba na kuwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu  badala yake katika hotuba yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -