IMEELEZWA kuwa siasa zisizo huru zinachangia kuongezeka kwa watu wenye upungufu wa akili duniani. Akiongea na gazeti hili wakati wa mah...
Akiongea na gazeti hili wakati wa mahojiano maalumu,
Mwanasaikolojia mwandamizi na Mkurugenzi mtendaji Huduma ya Bado liko tumaini
inayohusika na vijana Elisha Kazimoto ambaye
pia ni Mwalimu Sekondari ya Muleba mkoani Kagera alisema kuwa ongezeko la watu
aina hiyo imekuwa ikiongezeka kila uchao.
“Siasa zisizo huru ndugu mwandishi zimeendelea kubana uwezo
wa mtu kuwa huru kifikira na kushusha uwezo wa kufanya maamuzi sahihi” Alisema.
Wakati huohuo Kazimoto alieleza kuwa kundi lililoathiriwa
zaidi ni Rika ya vijana na Wana ndoa na
kwamba Kisaikolojia ongezeko au upungufu
wa akili haitegemei akili ya utahila na darasani kwa kufaulu mitihanihuku
akibainisha kipimo cha akili ni Uwezo wa kufanya maamuzi sahii, muda, eneo na
kwa kusudi sahii.
Ametaja sababu zingine zinazoweza kuathiri Mfumo huu kuwa ni
pamoja na vitu mbalimbali zijulikanazo kama misukumo ya ndani, nje na mazingira
“Mifumo ya kimaisha kuwa migumu, ya kimapenzi na ndoa
kuchanganya, Uchumi kuwa mgumu, huchangia kuvuruga mfumo wa tafakari ya kina kwa
kutoa maamuzi sahii”
Ameishauri jamii na Serikali kwamba kutenge kada hii au
iirasmishe, pamoja na wanao hitimu vyuo vikuu kupewa ajira moja kwa moja katika
taasisi mbalimbali za kiserikali, mahospitali, maofisi ya umma, na NGO's ili kupunguza
majanga mengi ya kisiasa,kijamii na kiuchumi.
Kutumia vizuri
Teknolojia, Elimu na kutoshiriki masuala ya kishirikina na kuweza kutumia
rasilimali za taifa hasa tunapoelekea katika uchumi wa Tanzania ya viwanda
COMMENTS