WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Ta...
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa
Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka
2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia.
Lengo
la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata
takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya
makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.
Dk.
Mpango alisema kuwa Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya
umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013
hadi sasa.
“Takwimu
zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua
kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dk.
Mpango.
Alisema
pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba
Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha kuwa
kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi unavyokua
hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.
“Nimefurahi
kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa
Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kupitia zoezi
hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana wapata 620 katika
maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dk. Mpango.
Aliwaasa
wadadisi hao kufanyakazi zao kwa umakini na weredi mkubwa ili takwimu
zitakazopatikana ziwe sahihi na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia
hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuvuruga zoezi hili.
Awali,
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa alieleza kuwa
ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi
utafanyika katika maeneo 754 yaliyochaguliwa kitaalamu kwa kutumia takwimu za
Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.
“Utafiti
huu utakuwa wa saba tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961, ambapo tafuti
nyngine zilifanyika 1969, 1991/92, 2001, 20117 na mwaka 2011/12” aliongeza Dk.
Chuwa.
Alisema
kuwa utafiti huo mpya utafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ijulikanayo
kama Survey Solution (CAPI) na kwamba matokeo ya awali ya utafiti huo
yanatarajiwa kutolewa ndani ya miezi sita ijayo ili nchi iweze kufahamu kiwango
cha umasikini uliopo katika jamii hivi sasa baada ya kufanyika kwa utafiti kama
huo miaka mitano iliyopita.
“Utafiti
wa mwisho uliofanyika mwaka 2011/2012 uliotumia karatasi uligharimu shilingi
bilioni 20 lakini kwa kutumia teknolojia mpya, utafiti huu utagharimu kiasi cha
shilingi bilioni 10 pekee” alisisitiza Dk. Chuwa.
Dk.
Chuwa alisema kuwa anaamini matokeo ya utafiti huo yatakuwa chachu ya kupata
takwimu za msingi kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa program
mbalimbali za kitaifa na kimataifa zenye kulenga kupunguza kiwango cha
umasikini nchini.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu ya
TEHAMA
COMMENTS