Habari Mpya

Saturday, 18 November 2017

KARIBU mwanandoa na wachumba mwenzangu katika safu hii tubadilishane mawazo na kujuzana mambo kadhaa kuhusu masuala ya ndoa, uchumba na mafanikio na changamoto zake.

Leo tutazungumzia mambo muhimu ya kuzingatia kwa wale walio katika uchumba kabla ya kufanya maauzi ya kufunga ndoa na mpenzi wako wadhati upendaye.

Fanya  haya kabla ya kuingia katika ndoa kipindi cha mahusiano ya uchumba kwa muktaza wa kuwa mke au mume. Kwa pamoja fanyeni maamuzi ya kupima afya zenu magonjwa ya Kaswende, Homa ya ini,Ugonjwa wa ukimwi,Gonorea ili kufanya maamuzi sahihi ikitokea mmoja ameathirika na kuamua kuwa pamoja au kuachana.

 Ugonjwa wa kaswende. (Syphilis)
    Kitaalamu  unajulikana  syphilis  huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu.Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiana na huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi katika sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri.hadi kufikia hatu kuwa tatizo kwa mhusika.

Aidha kidonda hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kuwa kichaa.

 Ugonjwa wa hepatitis B (Homa ya ini).
    Ugonjwa huu ni hatari sana  na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi  kuambukizwa  ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi.

   Aidha hushambulia mwilini sehemu ya  maini  na  kuacha  makovu, Mgonjwa macho huwa ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa hii mwishoni  husababisha kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.

Ugonjwa wa ukimwi.(HIVS)
    Huu ni ugonjwa unaofahamika kwani umeatangazwa sana hasa kwenye vituo vya Radio, Tv, Magazeti,majalida na sehemu mbalimbali hapa nchini. Ili kuelimisha  jamii. Tafiti inaonyesha uligundulika karne ya 20,hadi sasa umeshaua watu wengi sana zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa ni  kwa kushiriki ngono bila zembe kinga.

Ugonjwa wa gonorea.
     ugonjwa huu wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote  kwa wanaume na  wanawake, mara nyingi Mwanaume hawezi kujificha akiupata ugonjwa huu sabababu dalili za ugonjwa huo  ni kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea (tupu) ya  mwaname hivyo hubaini mapema ,kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa muda na mwanamke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujijua.mwisho ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba.


    Ushauri , (wapenzi ) wachumba wanawajibika kujali afya na kupata ushuri kwa wataalamu wa afya na wanasaikolojia mapema  kabla ya kuingia katika ndoa ili  matatizo yote yamalizwe kwa  ushauri na kumpa mawazo chanya inasaidia sana kumfanya  mme na mke kuwa na furaha kuwa nawe.Ingawa  Ndoa za vijana wa sasa hawazingatii na kujikuta wakiwa katika majuto kwa kukurupuka  kuja kubaini tatizo baadaye, ni vitu  muhimu sana vihusuvyo  wanandoa,wachumba licha ya kujuana  wengi na wengine walioko kwenye mahusiano hawajui na kwa hivyo kujikuta wanakutana na wakati mgumu hatimaye kuwa na migogoro ,michepuko inaanza.   

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -