WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa Ka...
WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia,
Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha
aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu, Tuangoma Jijini Dar es Salaam.
Yahya Msulwa |
Msulwa amefariki
dunia Alhamisi, Novemba 16, 2017 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es
Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika maombolezo hayo Waziri Mkuu
ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo
hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa
kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.
Amesema kuwa marehemu
alikuwa mchapakazi na mwenye ushirikiano mzuri na wenzake, ambapo Novemba 12,
2017 alipokea barua kutoka CWT iliyosainiwa na marehemu akimualika kushiriki
kwenye shughuli za chama.
“Wote tumeguswa na
msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa Chama cha Walimu Tanzania
tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa kila mmoja. Alikuwa na tabia
njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema aliyotuachia”
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu
Jijini Dar es Salaam
COMMENTS