WATU 40 wa Kitongoji cha Isumbi katika Kijiji cha Igung’hwa Kata ya Kinaga katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, wamelazwa ...
WATU
40 wa Kitongoji cha Isumbi katika Kijiji cha Igung’hwa Kata ya Kinaga katika
Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, wamelazwa katika Hospitali ya
Wilaya hiyo baada ya kudaiwa kula kiporo na mboga za majani aina
ya mgagani.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Kinaga, Paul Damasi alisema wananchi waliolazwa katika
Hospitali ya Mji wa Kahama ni wale waliokula kiporo cha ugali na mboga za
majani aina ya mgagani waliouita “mchicha.”
Aliyasema
hayo juzi wakati akizungumza na wananchi katika msiba uliotokea nyumbani kwa
Salum Manyanda na kuongeza kuwa asilimia kubwa ya watu waliougua ghafla baada
ya kula chakula hicho ni wanawake.
Ofisa
Mtendaji wa Kata huyo alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi baada
ya waombolezaji kula chakula kilichobakia jana ya siku hiyo huku akieleza kuwa
wote waliougua ghafla walikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama
kupatiwa matibabu.
“Idadi
ya watu haijafahamika ila nimepewa taarifa kuwa ni zaidi ya wakinamama arobaini
ndiyo waliokimbizwa katika Hospitali ya Mji wa Kahama, msiba ulitokea Novemba
14, kama unavyojua vijijini bado kuna ile tabia ya msiba unapotokea akinamama
wanapika chakula nyumbani kisha wanapeleka msibani.
COMMENTS