Powered by Blogger.

About

[Michezo kimataifa][column2]

Labels

Blog Archive

Search This Blog

Blog Archive

[random][featured1]

BTemplates.com

MICHEZO KITAIFA

[michezo][column2]

Blogroll

[afya][fbig2]

Contact us

Name

Email *

Message *

BTemplates.com

Yunus kijana anayetoa funzo kwa wenzake kujikwamua

KILA mtu ana ndoto ya kufikia lengo fulani   katika maisha yake. Na hapo ndipo hutimia neno la kitaalamu lisemalo: ‘Maandalizi ya leo ni ma...

KILA mtu ana ndoto ya kufikia lengo fulani  katika maisha yake. Na hapo ndipo hutimia neno la kitaalamu lisemalo: ‘Maandalizi ya leo ni mafanikio ya kesho’ au maisha ni mchakato, hatua’.



Kijana Joas Yunus kwa muda mrefu amekuwa na ndoto ya kuwa mwandishi wa wa vitabu kwa ajili ya kuielimisha jamii kupitia fasihi andishi iliyoianza tangu akiwa mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Nzovwe iliyoko wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.

Anasema tangu akiwa darasa la nne alipenda kufundisha japo hakujua atafundisha kwa njia gani, hivyo aliamua kujitolea kuwafundisha wanafunzi wenzake walio madarasa ya chini yake, baadaye kuanzisha kituo cha mafunzo kwa watoto wadogo ambacho aliendelea nacho hata baada ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2003.

Alisema ili kutopoteza ndoto yake, aliendelea kujitolea kuwafundisha hata baada ya kuendelea na masomo ya sekondali ingawa alipatwa na changamoto nyingi kwa kuwa haikuwa rahisi kuwafundisha aliokuwa anasoma nao darasa moja na wakamkubali wote.

Hata hivyo, pamoja na changamoto alizopata hakukata tama na alipohitimu sekondari aliendelea kufundisha masomo ya jioni katika kituo alichokianzisha nyumbani kwao kabla ya kupata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Pugu mwaka 2008.

Baadaye alipogundua kwamba kufundisha kuna tija kwa jamii, akaamua kuwashirikisha baadhi ya wenzake ili kuandika vitabu.

Aligundua kwamba ili vitabu viwe bora, kusomwa zaidi na kuongeza soko anatakiwa atafute watu wenye uwezo wa kusanifu hasa upande wa marafiki zake.

Ubunifu wake huo ulimsaidia kuongeza kipato na kufanikiwa kupata mtaji wa kuzalisha matoleo mengine zaidi huku akiendelea na masomo yake pamoja na kuendeleza kituo chake alichokuwa amekianzisha mkoani Songwe hadi alipoanza elimu ya juu.

Anasema aliendelea na kituo chake hicho  na kufanikiwa kugawa mtaji kwa kuanzisha kituo kingine cha elimu kwa vijana na watu wazima pasipo gharama zozote kwa nia ya kuisaidia jamii yake.

Baada ya kurudi kijijini kwao alifanya ibada zake katika kanisa la FPCT na kuchaguliwa kuwa katibu wa vijana kanisani baada ya kumpenda kutokana na uandaaji, uandishi na mpangilio mzuri wa taarifa za vikao vya kanisa.

Kazi yake ya kuisaidia jamii ikamfanya apate umaarufu zaidi na kuchaguliwa kuwa katibu wa vijana katika kanisa la FPCT alilokuwa akifanya ibada.

Yunus alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2010 na kupata Shahada ya Sayansi ya Kompyuta  na baadae elimu mbalimbali ya ujasiriamali.

“Pia nilifanikiwa kusoma shahada ya elimu sayansi ya kompyuta na baadaye ujasiriamali. Niliweza kusoma na kufanya kazi zangu kuhakikisha tu kwamba vitabu vipo katika usahihi,” alisema.

Anasema akiwa katibu alipata wazo jingine katika kutoa huduma kwa vijana wengine nje ya kanisa hivyo akamua kusajili kitabu chake alichokiita ‘Kijana jitambue’  kilichokuwa na maudhui ya kutoa elimu mbalimbali kwa rika ili waweze kujitathmini na kujitambua hasa katika kuziona fursa mbalimbali na kuzichangamkia.

Mwaka 2015 aliandika kitabu kingine alicho kiita ‘Inuka’ kwa maana ya inuka katika dimbwi la umasikini na kujifunza ufundi wa magari mtaani.

Anasema alikuwa hana uhakika wa kupata kazi, jambo lililomsukuma kubuni njia ya kupata kazi. Anasema aliamua kupanga makopo matupu ya oili pembeni mwa barabara ya zamani ya Bagamoyo ili kuwavuta watu walioharibikiwa na magari.

“Ndipo siku moja, raia mmoja wa kigeni akaona yake makopo na kushuka kutoka ndani ya gari. Kisha nilimsogelea na kugundua kuwa gari yake ilikuwa na hitilafu iliyosababisha isiwake, niliitengeza na kulipwa pesa ambayo kwangu ilikuwa mtaji,”anasema.

Anasema changamoto zilizopo katika kazi yake ya uandishi ni pamoja na kutokuwa na watu wanaoweza kumuwezesha pamoja na kukosa vitendea kazi kama vile kompyuta
Yunus kwa sasa meamua kujiajiri kupitia fani yake ya uandishi wa vitabu na kuwashauri waandishi wengine kuandika kwa ajili ya jamii na Tanzania ya viwanda iweze kuendelea mbele pamoja na kuanzisha  vituo vingi vya kutoa mafunzo kwa vijana katika kila wilaya.


COMMENTS

[facebook]
Name

AFYA,6,GURUDUMU LA MAISHA,2,HABARI,48,KIJIJINI,7,KIMATAIFA,9,MAHUSIANO NA SAIKOLOJIA,2,MAKALA,2,MAKALA YA ELIMU,1,MICHEZO,2,MIKOANI,4,SARAFU,4,VIDEO,4,ZANZIBAR,1,
ltr
item
LENZI MEDIA: Yunus kijana anayetoa funzo kwa wenzake kujikwamua
Yunus kijana anayetoa funzo kwa wenzake kujikwamua
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpDGbkzg1dQiY0Hb45Ku7BHPsbOL4I_0UDQeSYX6gGcqOS0_zh-CrqrTFFtOMES9YsINNeKR0zlZXD3mTWLliTi6eRK7o8DK-vfeJsvZGjRxsRFBZx_FORWIRX9YezTRsDs-Too1Gdnn4/s640/JOUAS.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpDGbkzg1dQiY0Hb45Ku7BHPsbOL4I_0UDQeSYX6gGcqOS0_zh-CrqrTFFtOMES9YsINNeKR0zlZXD3mTWLliTi6eRK7o8DK-vfeJsvZGjRxsRFBZx_FORWIRX9YezTRsDs-Too1Gdnn4/s72-c/JOUAS.jpg
LENZI MEDIA
https://lenzimedia.blogspot.com/2017/11/yunus-kijana-anayetoa-funzo-kwa-wenzake.html
https://lenzimedia.blogspot.com/
https://lenzimedia.blogspot.com/
https://lenzimedia.blogspot.com/2017/11/yunus-kijana-anayetoa-funzo-kwa-wenzake.html
true
2372332392983471599
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content