Habari Mpya

Habari Zote

Showing posts with label AFYA. Show all posts

TAFITI zinaeleza kuwa zipo baadhi ya dalili zinazojitokeza katika mwili wa binadamu ambazo katika hali isiyo ya kawaida ni ishara kuwa mwili huo una shida na unahitaji uchunguzi kugundua ni tatizo la aina gani. 

Baadhi ya dalili hizo zilizoelezwa na tafiti hasa kwa watoto wadogo zinazoashiria kupatwa na ugonjwa wa saratani ni kuvimba sehemu ya mwili bila maumivu yoyote  hasa sehemu za  shingo, miguu, shavu na tumboni.

Akizungumza na Raia Tanzania mapema wiki hii, Katibu wa Shirikisho la Vyama  vya Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala (SHIVYATIATA),  lenye makao yake Tabaa Relini Jijini Dar es Salaam Dk. Othuman Shem alisema baadhi ya dalili katika mwili wa binadamu  ni ishara ya ugonjwa wa saratani ingawa kundi kubwa la watu halina ufahamu huo.

Dk. Shem ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha dawa za asili cha  Paseko Natural Clinic  alisema  utafiti uliofanywa na kampuni ya Paseko T.O & P. Co. Ltd  kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ireland  hapa nchini,  ulionesha kuwapo kwa kundi kubwa la watu katika hamii hasa watoto kuwa na dalili hizo bila kujua kuwa ni dalili za saratani hasa watoto.
Image result for picha ya mtoto mwenye uvimbe wa saratani
Picha ya mtoto mwenye uvimbe.

 “Katika hatua ya kuangalia dalili hizo kwa kushirikiana na ubalozi wa Ireland hapa nchini, tumegundua kuwa zaidi ya asilimia 67 ya dalili hizi inaonesha kuwa huu ni ugonjwa wa saratani lakini wengi  hawajui.”alisema Dk. Shem.

Aliendelea kusema kuwa dalili zingine ni pamoja na mtoto  wa jicho kuwa na rangi nyekundu, makengeza na hata upofu wa ghafla.

“Pia damu kutoka kwenye fizi, kuvia katika macho, kutapika wakati wa asubuhi, kuumwa na  kichwa kupitiliza, kukonda bila sababu, kupungua uzito, homa inayojirudia rudia bila kuwa na chanzo, nguvu ya mwili kupungua kuliko kawaida” alisema. Othuman.

Zaidi ya dalili hizo, nyingine ni  mtoto  kupungua damu mwilini mara kwa mara, alisema na kuongeza: “Tunaendelea kufanya tafiti zaidi ili kuweza kuokoa  Watanzania, hii ni pamoja na kutoa elimu hasa vijijini ambako wengi wanakuwa na dalili hizi lakini hawazijui na kujikuta wakipoteza maisha ama watoto au wapendwa wao,”aliongeza.

Kwa muktadha huo, alisema kampuni  hiyo  imeamua kujitolea  kwa kushirikiana na mamlaka zingine kupima bure watoto wenye  dalili hizo nchini kote na kusema kuwa milango iko wazi kwa Mtanzania mwenye hitaji 
WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM  yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile

“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa hada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dk. Ndugulile.

Amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

Mbali na hayo Dk. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya  imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba Dk. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.

“Wahitimu waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema.

Mbali na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.


Naibu Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Ndugulile  alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya fani mbalimbali katika  kada mbalimbali za sekta ya afya.
JAMII imeshauriwa kujiunga kwenye vikundi ili kuunganishwa kwenye mfumo wa teknolojia ya usafishaji wa  maji taka kwa ajili ya matumizi mengine ili mfumo huo uwasaidie kutumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali zenye tija badala ya kuyateketeza baada ya matumizi.
Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya maji taka (OSWAMS), Juma Mohamed Nasoro (aliyevaa shati la zambarau wanne mustari wa mbele) akiwaonyesha maofisa wa serikali namna teknolojia ya uthibiti wa maji taka unavyofanya kazi jijini Dar es Salaam hivi karibuni (PICHA:  JAMANDA FUMBA).

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya maji taka (OSWAMS), Juma Mohamed Nasoro katika ziara ya maofisa mbalimbali wa serikali  walipokuwa wakitembelea mradi huo unaotekelezwa katika nyumba za maofisa wa jeshi la polisi,  mikocheni jijini Dar es Salaam.

Alisema tekonolojia ya usafishaji wa maji taka ni muhimu wakati huu taifa likihitaji watu wake kuwajibika ipasavyo kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji  mali kufikia uchumi wa kati kwa njia ya viwanda.

Kwa bahati mbaya, sehemu kubwa ya watu hawajatambua fursa zilizopo katika matumizi ya teknolojia hiyo na kusababisha maji taka yanayozalishwa  kuteketezwa wakati yangetumika kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji wa samaki, ujenzi na bustani.

“Maji machafu ni fursa sio tatizo. Kwa hali ilivyo sasa kila hitaji la maji lazima yatumike maji ya Dawasco. Tunataka maji taka yasafishwe na yatumike kwa shughuli za kuongeza kipato sio kutegemea maji ya Ruvu chini na Juu. Ili kufikia malengo haya ni lazima elimu ipelekwe kwa wananchi ya umuhimu wa teknolojia hizi ambayo pia huzuia magonjwa hasa ya mlipuko,”alisema.
Akifafanua kuhusu mfumo huo wa kutibu maji taka, Nasoro alisema kabla ya maji hayo kutumika hupitia hatua kadhaa kuanzia utengenezaji wa chemba ambayo ni ya kwanza ya matibabu ya maji hayo.

Kisha maji taka hupitishwa kwenye mfumo  wa pili wa tiba unaojulikana kitaalamu kama anaerobic (ABR) na U-Flow Anaerobic (UAF ) ambapo wadudu hula takataka kabla ya kufikia kiwango cha juu cha udhibiti, alisema.

“Maji yanayotibiwa kwa njia hizo yanakuwa yametibika kwa asilimia 85 na kiasi kingine huenda aridhini. Kwa hali hii sio rahisi kusababisha magonjwa, ni salama kwa matumizi kwani yamesafishwa kitaalamu. Yanafaa sana kwa kilimo na ufugaji kwani yana mbolea, nitrogen na phosphorus,”alisema.

Alisema kampuni yake imefanikisha teknolojia hiyo katika taasisi za umma na shule binafsi ya Libermann ya pia ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya maofisa waliotembelea mradi huo kutoka wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,  Jiji la Dar es Salaam na Manispaa za Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo waliridhishwa na utekelezwaji wa mpango huo na kusema hatua inayotakiwa ni jamii kuhamasishwa kujiunga baada ya kuutathimini na kuingizwa kwenye mipango ya ya serikali.

Afisa afya wa Manispaa ya Ubungo Wilson Msangi alisema teknolojia hiyo ni hupunguza gharama ya ukusanyaji wa maji taka, huchukua nafasi ndogo na kushauri Halmashauri kuihamasisha kwenye maeneo kama shule na hospitali kutokana na maeneo hayo kuzalisha kiasi kingi cha maji taka.

`Maji ya chooni ni dili’


·       Yamo kisukari, saratani, presha, hamu ya tendo

MMEA wa bamia uzaao matuda yanayoliwa, ni zao linalostawi karibu maeneo yote hapa nchini, ingawa hustawi na hupedwa zaidi na watu wa ukanda wa Pwani. Huliwa kama mboga kwa matunda hayo kupikwa yakichanganywa na aina nyingine ya mboga kama vile nyama.

Watu wa ukanda wa Pwani hutumia bamia kwa kuikatakata vipande vidogo na kuchanganya vipande hivyo na  majani ya maboga, magadi kisha kupika pamoja na kupata mboga iitwayo mlenda au hombwe kwa watu wa pwani ya mkoa wa Tanga.

Kwa bahati mbaya sana walaji wengi hawajui umuhimu wake kifya kama anavyobainisha Mtaalamu na Mkufunzi wa Chuo cha Tiba na Uuguzi ( IMTU) cha jijini Dar es salaam, Dk. Daniel Elifariji Mtango.

Mtaalamu huyo wa kitengo cha Afya na Jamii Chuoni hapo, anasema tunda la bamia lina vitamini A na B ambavyo huimarisha macho kutokana na  virutubisho hivyo kusheheni kiasi kingi cha protini ukilinganisha na lishe nyingine inayotokana na mimea.

Kama hiyo haitoshi, viini lishe vilivyomo husaidia kuwaokoa watoto  wenye  tatizo la utapiamlo, isulini kufanya kazi hivyo kuwaondoa watu katika hatari ya ugonjwa wa kisukari kwa  kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.

Zinapoliwa kwa usahihi, huongeza kinga za mwili kwa watoto na watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka na kuwa kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababishwa na kushuka kwa kinga ya mwili, anasema.

Akifafanua zaidi, Dk. Mtango anasema, maji ya bamia husaidia kuzuia magonjwa ya moyo kwa kuifanya mishipa ya damu kufanya kazi vizuri kutokana na maji yake kuwa  uwezo  wa kuondoa lehemu kwenye kuta za mishipa ya damu.

“Lehemu zisipoondolewa kwenye mishipa hiyo husababisha msukumo wa damu kwenda vibaya na kuwa chanzo cha maradhi ya shinikizo la damu. Kwa hiyo tunaona ni kwa jinsi gani ambavyo mmea huu ulivyo muhimu katika lishe na kudhibiti magonjwa ambayo wakati mwingine hayawezi kutibiwa hapa nchini. Hivyo bamia inaweza kupunguza idadi ya watu kwenda India kutibiwa maradhi ya moyo,”anasema,

Faida zingine za ulaji wa bamia  ni kuzuia tatizo la watoto kupasuka uti wa mgongo au mgongo waz, kumsaidia mama mjawazito pamoja na mtoto  tumboni  kuwa na afya  na baada ya kujifungua.
Hutibu tatizo la  kuchoka bila sababu, zaidi  kwa watu ambao wana msongo wa mawazo ambao mtaalamu anashauri kundi hilo kula kwa wingi bamia kwani huleta matokeo ya haraka na kufanya afya zao kuimarika zaidi na kuwafanya  wawe na amani, furaha muda wote.

Faida nyingine, hutibu vidonda vya tumbo na kuthibiti bakteria  wasababishao matatizo hayo na kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo, huongeza kiwango cha uzalishaji wa damu kwa wingi mwilini.

Huimarisha nywele na kuzifanya ziwe na muonekano mzuri pamoja na kufanya utumbo mpana kubaki katika ulaini wa asili yake  na kukinga mtumiaji dhidi ya  saratani ya utumbo mpana (large intestine).

Pia hufanya mfumo wa usagaji wa chakula kuwa mzuri na hivyo kupunguza maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa kutokana na majimaji ya bamia hulainisha choo kama ilivyo papai na ndizi mbivu. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa.

MATUMIZI:
·         Mlaji anaweza kupika bamia kama mboga kisha kuchanganya na chakula kingine na kula kama mlo. Vyakula hivyo vinaweza kuwa, uji, mchuzi, na vingine.

·         Matumizi mengine ni mtumiaji anatakiwa kukatakata bamia vipande vidogovidogo baada ya kuoshwa kwa maji safi na salama. Loweka kwenye maji kwa dakika kadhaa vipande hivyo kulingana na uwingi wa vipande vyenyewe ili kupata juisi.

·         Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha juisi ya bamia sawa na gramu 100. Au unaweza kula vipande hivyo vibichi vilivyojazwa kwenye kikombe cha ujazo huo .

·         Inashauriwa kuwa watoto wadogo wapatiwe  zikiwa zimepikwa.  Fanya hatua hizo tatu kwa mfululizo na matokeo yake hujitokeza kuanzia juma la tatu au kabla.


Anatoa ushauri kwa wakulima kulima zao hilo kwa wingi kutokana na faida hizo za kiafya na kukifanya kilimo chao kuwa na tija.

Ni zao linalokomaa kwa muda mfupi na hukabiliana na hali zote za hewa. Pia jamii kula kwa wingi bamia ili kupunguza matatizo ya kiafya  ambayo baadhi yake ameyaanisha katika makala haya.
BOGA ni moja kati ya matunda yenye faida mbalimbali katika mwili wa binadamu. Hupatikana karibu mikoa yote ya Tanzania, na idadi kubwa ya watu wengi kulima boga kwa matumizi ya nyumbani kama chakula.

Wengi pia hawajui faida za tunda zaidi ya kulitumia kama chakula, lakini ukweli ni kwamba matumizi yake ni zaidi ya chakula.

Boga huweza kusindikwa au kusagwa na kupatikana kimiminika (juisi) muhimu kwa afya ya binadamu kwani hutibu magonjwa mbalimbali.

Dk. Othman Shemu ni mtaalamu wa miti na mimea dawa na Mkurugenzi mtendaji wa kliniki ya tiba asili cha Paseko yenye makao yake Tabata relini Jijini Dar es Salaam, anasema juisi ya boga pia huimarisha na kuongeza nguvu za kiume.

Huwafanya wanaume kumudu tendo la ndoa hasa wale ambao huishia mshindo au pigo moja au kushindwa kumfikisha kileleni mwanamke na wakati mwingine kukosa hamu ya tendo la ndoa Anasema tunda la boga lina protini na virutubisho mbalimbali vyenye uwezo wa kutibu magonjwa ikiwamo kutengeneza mbegu za kiume kwa wingi kama ilivyo baadhi ya vyakula vya protini.

Baadhi ya magonjwa hayo ni tezi dume, kusafisha figo, tatizo la kutapika mfululizo hasa kwa mama mjamzito, huondoa tatizo ya gesi tumboni na msongo wa mawazo.
“Ukitunia juisi hii huruhusu ubongo kuingiza hewa safi kwa wingi (oxgen) na kutoa hewa chafu hali inayofanya ubongo kuwa mwepesi na kutunza kumbukumbu za kutosha, “ anasema Dk Shemu.

Pia huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuondoa vijidudu visivyotakiwa tumboni, pamoja na kusaidia kurekebisha mfumo wa msukumo wa damu kwa watu wenye matatizo ya presha.

Huweza kutumiwa na rika za watu wote ingawa ni muhimu zaidi kutumiwa na watoto kwani huwakinga na magonjwa na kuwasaidia kujenga uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu (akili) jambo ambalo linaweza kuongeza ustawi wa masomo darasani.
UANDAAJI:

Shemu ambaye pia ni katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Waganga (SHIVYATIATA) anasema zipo njia mbalimbali za uandaaji wa ambapo mhussika anasema kumenya maganda ya juu yasiyotakiwa kisha maandalizi kuanzia nyama (sehemu ya njano), moyo na mbegu.

Chukua nyama, kata vipande vidovidogo baada ya kusafishwa kwa maji safi na salama. Jaza vipande hivyo kwenye mashine maarufu kama (Brenda) kwa ajili ya kusaga au kusindika.

Unaweza wakati wa kusindika unaweza kuchanganya vipande hivyo na ndizi, maji safi kidogo ili kurahisisha usindikaji kutokana na ndizi na vipande vya boga kuwa katika hali kavu.

Inashauriwa kuwa juisi iliyosindikwa katika mchanganyiko huo ina ongezeko kubwa la virutubisho kama vile kalishiamu husaidia watu wenye upungufu au ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI) kuongeza kinga ya mwili.

“Pia majaribio yetu yameonyesha kwamba juisi hii ikichanganywa na juisi ya maua yajulikanayo kama rosemary maarufu kama rosella inakuwa na uwezo zaidi katika tiba kutokana na virutubisho vingine kama kalishiam na magnesiamu vilivyomo kwenye rosella,”alisema.

Zipo aina mbalimbali za uandaji wa juisi ya boga kwa mtu mwenye tatizo la nguvu za kiume hutakiwa, kuchukua boga na kulikata vipande vidogo vidogo na kusaga bila vipande hivyo kuwa mbegu zake.

Anachotakiwa mhusika kufanya ni kuzipaa mbegu za boga ili kuzitenganisha na nyama kisha kuzianika sehemu yenye kivuli hadi zitakaponyauka, saga kwa ajili ya kupata unga.

Inashauriwa kusaga unga huo wakati wa matumizi tu kwani unga wake ukihifadhiwa muda mrefu unaweza kusababisha mlundikano wa fangasi ambao ni hatari kiafya, alisema Dk. Shemu.

MATUMIZI:
Unaweza kunywa juisi ya boga iliyosindikwa na kuchanganywa na pensheni ili kuongeza ladha (test) na sukari kidogo kadri unavyoweza kwasababu matumizi yake mengi hayadhuru.

Kuhusu unga wa mbegu za boga, mtumiaji mwenye matatizo hayo anatakiwa kuchukua unga kwenye kijiko kimoja cha chai kisha kuchanganya kwenye glasi ya maji na kunywa.


“Kunywa mara tatu kwa siku. Mwneye tatizo kubwa anapaswa kunywa katika muda wa siku 21 mfululizo. Kwa mwenye tatizo la msongo wa mawazo anaweza pia kunywa juisi ya mchanganyiko wa ndizi mbivu na boga kwa kuchanganya na unga wa mbegu hizo”alisema.
Kuna aina  nyingi  ya vyakula ambavyo ni bora kwa afya yako na
inaweza kukuepusha mbali na magonjwa kama moyo, kiharusi, na cholesterol.
Lakini katika kipindi cha miaka kadhaa, ugonjwa wa moyo umeshuka na ni kwa sababu watu walioathirika wanaongeza ya kuzingatia kanuni katika mlo wao.
Uchunguzi tofauti umegundua kuwa kwa kutumia hizi vyakula hivi, watu wanaweza kuepuka ugonjwa wa moyo au cholesterol ya juu.

Hapa katika makala hii, wataalamu wanagawanya orodha ya superfoods katika maeneo 10 ambazo ni bora kwa watu wote ambao wana shida ya moyo. Hizi superfoods zitakuzuia mbali na ugonjwa huu.

1.      Chai ya kijani

Uchunguzi wa hivi karibuni umegundua kuwa watu ambao hunywa chai ya kijani mara kwa mara wanaweza kujikinga na tatizo la ugonjwa wa kiharusi na magonjwa ya moyo.
 
Chai ya Kijani
Chai ya kijani ni utajiri na kuzuia sumu(antioxidants) iitwayo makatekini na polyphenols, ambayo inaweza kukuzuia mbali na tatizo la moyo pamoja na uharibifu wa seli.

Jaribu kuongeza chai ya kijani kwenye lishe yako kwa sababu itasaidia kimetaboliki yako na pia itaboresha afya yako ya moyo


2.      Maharagwe
Pulses au maharagwe ni bora zaidi kwa afya ya moyo pamoja na figo, pinto na Maharagwe meusi. 

Vipande hivi vina nyuzi ambazo ni bora kwa kupunguza cholesterol LDL na kukuweka mbali na tatizo la moyo. Unaweza kuyapata  maharagwe yote kwa urahisi katika maduka ya vyakula na gharama nafuu pia.


3.      SamakiFatty
Kuna samaki kadhaa ambao wana asidi ya mafuta ya omega-3 kama sahani, herring, bahari ya ziwa, anchovies, mackereli na sardini.


Omega-3 fatty asidi husaidia katika kupunguza hatari ya atherosclerosis (kuimarisha mishipa ya damu), arrhythmia ( na usawa wa mapigo ya  moyo) na triglycerides.

4. Viazi
Watu wengi huamini kwamba Viazi ni vina kiasi kikubwa cha kalori lakini si kweli. Viazi vina potashamu nyingi, vitamini B, folic asidi, kalsiamu, na nyuzi nyuzi(fiber).

Mboga hii husaidia katika kupunguza shinikizo la damu. Pia hupunguza hatari ya ugonjwa wa kiharusi na moyo.


Hata ivyo wataalamu wanashauri kuwa ni vizuri kupika viazi pamoja na maganda ili kupata virutubisho vingi. Ngozi yake inazalisha seli kwa uwingi(antioxidant) na kupambana na vichocheo vya magonjwa.


5.      Chokoleti cha giza
Uchunguzi tofauti umeonesha kwamba kula chocolates giza itasaidia katika kupunguza hatari ya kiharusi na mashambulizi ya moyo.

Chokoleti ya giza imefungwa kwa kiasi kikubwa cha flavonoids ambacho kinajulikana kama polyphenols ambazo zinasaidia katika kutibu uvimbe, kuzuia mzunguko wa damu usiofaa na shinikizo la damu. Kwa hiyo wale watu ambao wanatumia chokoleti giza wanaweza kuepukana na magonjwa haya yote.


6.      Mbegu za Chia
Mbegu za Chia zinajumuisha omega-3 mafuta asidi ambayo ni nzuri kwa wanadamu wote, hasa kwa wagonjwa wa moyo. 

Omega-3 fatty asidi husaidia kupunguza hatari ya dalili za kawaida za moyo na pia kupunguza triglycerides katika damu. 

Chakula hiki pia hutajiriwa na nyuzi za mumunyifu, protini, antioxidants, chuma, kalsiamu, magnesiamu na madini.


7. Berries na matunda ya machungwa
Berries

Kuna berries nyingi sana, kama jordgubbar, berries acai, blueberries, nk. Berries hizi zote ni superfoods nzuri kwa afya ya moyo. Flavonoids, zinazopatikana katika berries hizi, husaidia kupunguza shinikizo la damu, kudumisha mzunguko wa damu pamoja na kupanua mishipa yako ya damu.

Blueberries na jordgubbar zina viwango vingi vya kinga ambavyo vinaweza kuzuia kuwepo kwa plaque pamoja na msaada katika kupanua mishipa ya damu katika mwili.


Matunda ya Citrus kama mazabibu na machungwa yana kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol na ugonjwa wa moyo.


8.      Kolilili, kale, broccoli
Kuna mboga nyingi ambazo zimejaa vitamini C kama vile kabichi, bok choy, kale, cauliflower, broccoli, kale, mchicha na vichaka vya brussels.

Hizi mboga zote za kijani husaidia kudumisha afya ya moyo wako na pia kukuzuia mbali na mashambulizi ya moyo na ugonjwa wa moyo. Mboga hizi zinabeba asidi ya mafuta ya omega-3, madini, nyuzi na vitamini.
Kwa hiyo jaribu kuongeza mboga zote za kijani katika mlo wako wa kila siku ili uondoe ugonjwa wa moyo.

9.      Karanga
Karanga kama macadamia, peanuts, walnuts, pistachios, na almond ni karanga zilizobeba nyuzinyuzi(fiber) ambayo ni nzuri kwa afya ya moyo.
Karanga hizi pia zina uwingi wa vitamini E ambayo husaidia kupunguza mafuta ya cholesterol mbaya. Baadhi ya karanga hizi kama pecans, cashews, walnut na almond ni zina omega-3 nyingi za mafuta ya asidi. Kwa hivyo kuongeza karanga katika mlo wako wa kila siku utakuweka mbali na ugonjwa wa moyo.
Aidha, pia hupunguza hatari ya fetma au unene uliopitiliza na kupunguza kiwango chako cha damu cha LDL (low density lipoprotein) ili kuzuia ugonjwa wa moyo.


10. Quinoa

Ni nafaka nzima (sawa na mchele wa kawaida mweupe, mchele wa kahawia na nafaka nyingine kama ngano na shayiri). Quinoa ni vyakula vya juu vya gluten. Ina madini na protini.
Yote 9 ya amino asidi muhimu hupatikana katika quinoa, ikiwa ni pamoja na lysine ambayo ni muhimu kwa ajili ya kukarabati tishu na ukuaji. Quinoa husaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo. Unaweza kuongeza quinoa katika muffins, saladi na supu.


Hii ni orodha kamili ya superfoods 10 ambazo zinaonekana kuwa nzuri kwa afya ya moyo. Vyakula hivi vyote hupatikana kwa urahisi katika masoko na pia ni gharama nafuu. Kula mara kwa mara ili kujilinda kutokana na ugonjwa wa moyo.

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -