KKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye hakufahamika kwa jina Amenusurika na kipigo na wananchi Wenye hasira kali mara baada...
KKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye
hakufahamika kwa jina Amenusurika na kipigo na wananchi Wenye hasira kali mara
baada ya kufanya Uharibifu kwa kuharibu mashine ya Kusaga mahindi ya
Mjasiliamali mwenzake kutokana na wivu wa kimaendeleo.
Kijana huyo mkazi wa kijiji cha Nyikonga wilayani
Mbogwe Mkoani Geita amenusurika na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali
mara baada ya kuvamia nyakati za usiku na kuanza kuharibu mashine ya kusaga mahindi
iliyo jirani yake inayotumia mafuta ambapo yeye ameajiriwa katika mashine inayotumia
Umeme.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa
serikali ya kijiji hicho Mperwa Sekela amesema kesi hiyo kwa sasa iko
mahakamani huku akitoa wito kwa wananchi
kuachana na vitendo vya kujichulia sheria mkononi.
Kwa upande wake mmiliki wa mashine hiyo iliyoharibiwa
hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo huku mmiliki wa mashine alikokuwa
anafanyia kazi kijana aliefanya uharibifu huo amekiri kutokuwa na ugomvi wowote
na jirani yake huku baadhi ya wananchi wakishangazwa na kitendo alichokifanya
kijana huyo.
Mpaka sasa kijana huyo yuko chini ya uangalizi wa
vyombo vya Dola katika hatua zaidi za
uchunguzi wa Tukio alilofanya.
COMMENTS