KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewakumbusha wananchi wa kijiji cha Vuchamangofi wanaohitaji kuwekewa umeme ghara...
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewakumbusha wananchi wa kijiji cha Vuchamangofi wanaohitaji kuwekewa umeme gharama zake ni Sh. 27,000 kwa vna sio vinginevyo kama ambavyo wamekuwa wakidanganywa
"Msikubali kutozwa
zaidi ya Sh.27,000 kwa sasa umeme sio hanasa, kila mtu anatakiwa kupata huduma
hii kwa gharama ya chini kwa sababu serikali imeamua kutoa huduma hii maeneo
yote nchini," amesisitiza Chongolo.
Chongolo ameyasema hayo
akiwa wilani Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa kwenye mwendelezo wa ziara ya
siku tano ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, miradi ya maendeleo na
kuhimiza sensa ya watu na makazi
Amesema kuna watendaji
wasio waaminifu wanawalaghai wananchi kulipa zaidi ya kiasi hicho.
COMMENTS