RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na maji katika maeneo mbalimbali nchini. Am...
RAIS wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na maji
katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema anatambua
matatizo yanayowakabili kina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo
muhimu hivyo Serikali itahahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 tatizo la maji
nchini linakuwa limekwisha.
Rais Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji wa Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Rais Samia ameyasema
hayo leo wakati akizindua mradi wa maji katika kata ya Makongorosi Wilaya ya
Chunya wenye thamani ya Sh2.5 bilioni utakaozalisha maji lita Milioni mbili kwa
siku.
Amesema katika ilani ya
uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ifikapo 2025 ilielekeza kutatua tatizo la
maji na kwa Mkoa wa Mbeya kuna miradi 50 ambayo imefikia asilimia 95 na ifikapo
2025 tatizo la maji litakwisha kwa asilimia 100.
Kwa upande wake, Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athon Sanga amesema mradi huo umefikia asilimia
70 ambao utazalisha lita milioni mbili zitakazo ondoa tatizo la maji katika
Wilaya ua Chunya.
Amesema wizara ina
mpango wa kuchimba visima vikubwa vya maji
katika mji wa Makongorosi ili kuondokana na hadha kwa baadhi ya maeneo
huku akimpongeza Mbunge wa Lupa, Masache
Kasaka kwa kutatua changamoto ya maji jimboni kwake kwa kuchimba visima.
Kwa upande wake, Mbunge
Kasaka amemuomba Rais Samia kusaidia kuboreshwa miundombinu ya barabara kutoka
chunya mpaka kijiji cha Itumbi ambako kuna shughuli za uchimbaji wa madini ili
kufungua fursa za kiuchumi.
Mchimbaji mdogo wa Madini
Kata ya Matundasi, Aden Mwakyusa amesema ujio wa Rais Samia ikawe chachu ya
changamoto za wachimbaji madini kutatuliwa pamoja na kuhodhi maeneo ambayo
yanashikiliwa na wachimbaji wakubwa.
CHANZO MWANANCHI
COMMENTS