Habari Mpya

Thursday, 4 August 2022

 

SERIKALI ya kijiji cha Lulembela wilayani Mbogwe Mkoani Geita imewatahadharisha baadhi ya watu wenye tabia ya kuwaficha watoto kisha kuanza kudai fidia kwa wazazi wao kwa kisingizio walikuwa wamepotea.

Kaimu Afisa Mtendaji Wa kijiji hicho PAUL NTAHENGAMA ametoa tahadhari kwa watu wenye tabia hiyo nakwamba wamekuwa wakipata taarifa kutoka kwa wananchi japo hawajabaini juu ya uwepo wa vitendo hivyo kwani wengi wanaowakota watoto hao huwaokota kwa nia njema na si kwa biashara.



kwa mujibu wa maelezo ya wananchi katika Eneo hilo wamedai wimbi la kupotea watoto kwa sasa ni kubwa nakwamba cha kushangaza pindi wanapowapata watoto hao huwalazimu kutoa fidia kuwakomboa kutoka kwa wasamalia wema waliowaokota jambo Ambalo wamehisi huenda kuna biashara ambayo inaendelea. Moja kati ya mzazi ambae amekumbana na changamoto ya mtoto wake kupotea nakulipishwa fidia amesema.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho MAISHA WILLIAM MAGINYA amesema Uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha watu wanaotumia Fursa hiyo ya kuficha watoto kujiingizia  kipato wameendelea kulifanyia kazi ili kubaini uwepo wa vitendo hivyo.

Katika hatua Nyingine Bw William amewataka wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao ili kuondokana na changamoto kama hizo kwakuwa wazazi wengi wamekuwa bize na uzalishaji mali nakusahau malezi kwa watoto.

NA NICHORAS PAUL LYANKANDO

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -