Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua maofisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kwa mujibu wataarifa iliyotolewa usiku w...
Rais wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan ameteua maofisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwa mujibu wataarifa iliyotolewa
usiku wa Jumamosi, Agosti 6, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Ikulu, Zuhura Yunus amefanya uteuzi huo juzi Alhamisi Agosti 4, 2022.
Miongoni mwa
walioteuliwa kuwa majaji wa Mahakama Kuu ni pamoja na Gabriel Pascal Malata
ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msajili
wa Mahakama ya Rufani, Kevin Mhina.
Majaji hao walioteuliwa
ambao tarehe ya kuapishwa itatangazwa ni;
1. Kevin David Mhina-
kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani
2. Gabriel Pascal
Malata-kabla ya uteuzi huu alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali
3. Adrian Philbert
Kilimi- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili Mahakama
4. Happiness Philemon
Ndesamburo- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;
5. Victoria Mlonganile
Nongwa- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama
6. Obadia Festo
Bwegoge- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama
7. Ruth Betwel
Massam-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama
8. Godfrey Ntemi
Isaya-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama
9. Gladys Nancy
Barthy-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama
10. Haji Suleiman Haji-
kabla ya uteuzi alikuwa Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar
11. Fatma Rashid
Khalfan-kabla ya uteuzi alikuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora
12. Abubakar A.
Mrisha-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Serikali
13. Lusungu Hemed
Hongoli-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali
14. Monica Peter
Otaru-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali
15. Kamana Stanley
Kamana-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi (Tamisemi)
16. Hamidu Rajabu Mwanga-kabla ya uteuzi
alikuwa Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi
17. Marlin Leonce
Komba-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
18. Dk Mwajuma Kadilu
Juma-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe
19. Dk Cleophas K.K.
Morris-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam
20. Asina A.
Omani-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
21. Aisha Zumo Bade-
kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea
22. Mussa Kassim
Pomo-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea.
Taarifa hiyo imesema
kuwa tarehe ya kuapishwa majaji hao wateule itatangazwa baaadaaye.
COMMENTS