BAADHI ya wafanyabiashara katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani geita mkoani Geita wamesema sheria kandamizi za ulipaji wa kodi i...
BAADHI ya wafanyabiashara katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani geita mkoani Geita wamesema sheria kandamizi za ulipaji wa kodi imekuwa kisababishi cha wengi wao kuingia katika vishawishi vya utoaji wa rushwa ili kuendelea na biashara.
Wakizungumza
katika moja ya kikao na maafisa wa Mamlaka ya Mapato TRA Wafanyabiashara hao
wametoa malalamiko yao juu Sheria kandamizi Ambazo zinawakandamiza
wafanyabiashara.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara CHARLES MAKANJI amesema TRA wamegeuka
kuwa chanzo cha kuwadidimiza wafanyabiashara kwa kuwatoza faini Ambazo
haziendani na mitaji yao.
Akitoa
Ufafanuzi wa suala la kodi Mwalimu Toa Elimu ya Kodi kanda ya ziwa LUTUFYA
MTAFYA amesema wao wanasimamia Sheria na Hawamkandamizi mfanyabiashara hivyo
amewaomba wawasilishe kero zao katika Ofisi za mamlaka hiyo na kero zao
kutatuliwa haraka iwezekenavyo.
Katika
Hatua nyingine akawaomba kutoziogopa Ofisi za TRA badala yake watumie ofisi hizo
kama kimbilio la kwanza kutatuliwa kero zao.
NA
NICHORAS PAUL LYANKANDO
COMMENTS