WAZIRI mkuu wa Tanzania KASSIM MAJALIWA amezindua mradi unaofahamika kama farm clinic wenye lengo la kuwezeshwa wakulima kufikia ajenda ya...
WAZIRI mkuu wa
Tanzania KASSIM MAJALIWA amezindua mradi unaofahamika kama farm clinic wenye
lengo la kuwezeshwa wakulima kufikia ajenda ya 10/30 yenye kauli mbiu ya kilimo
ni biashara kupitia farm clinic.
MAJALIWA amefanya
uzinduzi huo alipo tembelea maonesho ya nane nane jijini Mbeya huku akiwahimiza
vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo kwa kuwa serikali imeandaa mipango mingi
na mizuri kwa ajiri yao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa |
MAJALIWA amesema
kuwa anaomba kila mwananchi ajishughulishe na shughuli ambayo itamleta uchumi
ambayo itamsaidia kupata kipato ambacho kitamsaidia kila mtanzania kuendesha
familia.
Kwa upande wake
mbunge wa jimbo la mbeya mjini na spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania TULIA ACKSONI MWANSASU ametumia nafasi hiyo hiyo kumshukuru rais samia
suruhu hassani kwa kuleta mradi mkubwa wa maji ambao unaenda kumaliza
changamoto ya maji jijini Mbeya.
NA: ANYIGULILE
ZAKARIA
COMMENTS