Habari Mpya

Habari Zote

Archive for November 2022

 

KKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye hakufahamika kwa jina Amenusurika na kipigo na wananchi Wenye hasira kali mara baada ya kufanya Uharibifu kwa kuharibu mashine ya Kusaga mahindi ya Mjasiliamali mwenzake kutokana na wivu wa kimaendeleo.



Kijana huyo mkazi wa kijiji cha Nyikonga wilayani Mbogwe Mkoani Geita amenusurika na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali mara baada ya kuvamia nyakati za usiku na kuanza kuharibu mashine ya kusaga mahindi iliyo jirani yake inayotumia mafuta ambapo yeye ameajiriwa katika mashine inayotumia Umeme.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mperwa Sekela amesema kesi hiyo kwa sasa iko mahakamani huku  akitoa wito kwa wananchi kuachana na vitendo vya kujichulia sheria mkononi.

Kwa upande wake mmiliki wa mashine hiyo iliyoharibiwa hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo huku mmiliki wa mashine alikokuwa anafanyia kazi kijana aliefanya uharibifu huo amekiri kutokuwa na ugomvi wowote na jirani yake huku baadhi ya wananchi wakishangazwa na kitendo alichokifanya kijana huyo.

Mpaka sasa kijana huyo yuko chini ya uangalizi wa vyombo vya  Dola katika hatua zaidi za uchunguzi wa Tukio alilofanya.

 BAADHI ya Wananchi wa mtaa wa soko la wakulima kata Ruanda jijini Mbeya wamedaiwa kukumbatia watoto wanao fanya uharifu hali inayo pelekea kukithiri kwa vitendo vya uwizi ndani ya mtaa huo.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa huo mkutano uliokua unahusu namna ya kuuthibiti uharifu unao fanyika ndani ya mtaa wao.


Wananchi hao wamesema kuwa kuna umuhimu wa kurejesha ulinzi shirikishi ili kuweza kukabiria na vitendo vya uharifu vinavyo fanyika ndani ya mtaa.

Nae mwenyekiti wa mtaa huo ELIMGABI NJIBA ameagiza kuondolewa kwa vijana moja ya nyumba iliyopo mtaani hapo inayo daiwa kufuga vibaka.

Vitendo vya uwizi na udokozi vimeibuka kwa kasi hivi karibuni ndani ya mtaa huo hali iliyo walazimu viongozi wa mtaa huo kufanya mkutano na kupanga mikakati namna ya kukabiliana na uharifu unaofanyika ndani ya mtaa wao.

 


MBALAMWEZI

Serikali imesema kati ya taarifa 533 zilizopokelewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) mwaka 2021, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Felishi ameyasema hayo, leo Novemba 5, 2022 wakati akichangia taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali, (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.


Amesema wapo wanaotuhumiwa na waliobainika na wakachukuliwa hatua kulingana na sheria za utumishi.

“Inawezekana watu wanashangaa kuwaona watu mitaani, lakini yule mtu shauri lake limeshachunguza na tayari limeshafanyiwa kazi na mamlaka zinazohusika,” amesema.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ya mwaka 2021, kati ya taarifa walizopokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), 533, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko. Amesema taarifa 102 za CAG, zilichukuliwa hatua za kinidhamu na kwamba mchakato wa kutuhumiwa umegatuliwa Kikatiba.

“Inawezekana watu wakaonekana mtaani ameshafikishwa kwa muajiri na akatiwa hatiani kwa mujibu wa Sheria za Umma na Sheria ya Fedha za Umma,” amesema.

CHANZO: MWANANCHI

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -