Habari Mpya

Habari Zote

Showing posts with label AFYA. Show all posts

TAFITI zinaeleza kuwa zipo baadhi ya dalili zinazojitokeza katika mwili wa binadamu ambazo katika hali isiyo ya kawaida ni ishara kuwa mwili huo una shida na unahitaji uchunguzi kugundua ni tatizo la aina gani. 

Baadhi ya dalili hizo zilizoelezwa na tafiti hasa kwa watoto wadogo zinazoashiria kupatwa na ugonjwa wa saratani ni kuvimba sehemu ya mwili bila maumivu yoyote  hasa sehemu za  shingo, miguu, shavu na tumboni.

Akizungumza na Raia Tanzania mapema wiki hii, Katibu wa Shirikisho la Vyama  vya Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala (SHIVYATIATA),  lenye makao yake Tabaa Relini Jijini Dar es Salaam Dk. Othuman Shem alisema baadhi ya dalili katika mwili wa binadamu  ni ishara ya ugonjwa wa saratani ingawa kundi kubwa la watu halina ufahamu huo.

Dk. Shem ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha dawa za asili cha  Paseko Natural Clinic  alisema  utafiti uliofanywa na kampuni ya Paseko T.O & P. Co. Ltd  kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ireland  hapa nchini,  ulionesha kuwapo kwa kundi kubwa la watu katika hamii hasa watoto kuwa na dalili hizo bila kujua kuwa ni dalili za saratani hasa watoto.
Image result for picha ya mtoto mwenye uvimbe wa saratani
Picha ya mtoto mwenye uvimbe.

 “Katika hatua ya kuangalia dalili hizo kwa kushirikiana na ubalozi wa Ireland hapa nchini, tumegundua kuwa zaidi ya asilimia 67 ya dalili hizi inaonesha kuwa huu ni ugonjwa wa saratani lakini wengi  hawajui.”alisema Dk. Shem.

Aliendelea kusema kuwa dalili zingine ni pamoja na mtoto  wa jicho kuwa na rangi nyekundu, makengeza na hata upofu wa ghafla.

“Pia damu kutoka kwenye fizi, kuvia katika macho, kutapika wakati wa asubuhi, kuumwa na  kichwa kupitiliza, kukonda bila sababu, kupungua uzito, homa inayojirudia rudia bila kuwa na chanzo, nguvu ya mwili kupungua kuliko kawaida” alisema. Othuman.

Zaidi ya dalili hizo, nyingine ni  mtoto  kupungua damu mwilini mara kwa mara, alisema na kuongeza: “Tunaendelea kufanya tafiti zaidi ili kuweza kuokoa  Watanzania, hii ni pamoja na kutoa elimu hasa vijijini ambako wengi wanakuwa na dalili hizi lakini hawazijui na kujikuta wakipoteza maisha ama watoto au wapendwa wao,”aliongeza.

Kwa muktadha huo, alisema kampuni  hiyo  imeamua kujitolea  kwa kushirikiana na mamlaka zingine kupima bure watoto wenye  dalili hizo nchini kote na kusema kuwa milango iko wazi kwa Mtanzania mwenye hitaji 
WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM  yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile

“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa hada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dk. Ndugulile.

Amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

Mbali na hayo Dk. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya  imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba Dk. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.

“Wahitimu waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema.

Mbali na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.


Naibu Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Ndugulile  alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya fani mbalimbali katika  kada mbalimbali za sekta ya afya.
JAMII imeshauriwa kujiunga kwenye vikundi ili kuunganishwa kwenye mfumo wa teknolojia ya usafishaji wa  maji taka kwa ajili ya matumizi mengine ili mfumo huo uwasaidie kutumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali zenye tija badala ya kuyateketeza baada ya matumizi.
Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya maji taka (OSWAMS), Juma Mohamed Nasoro (aliyevaa shati la zambarau wanne mustari wa mbele) akiwaonyesha maofisa wa serikali namna teknolojia ya uthibiti wa maji taka unavyofanya kazi jijini Dar es Salaam hivi karibuni (PICHA:  JAMANDA FUMBA).

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya maji taka (OSWAMS), Juma Mohamed Nasoro katika ziara ya maofisa mbalimbali wa serikali  walipokuwa wakitembelea mradi huo unaotekelezwa katika nyumba za maofisa wa jeshi la polisi,  mikocheni jijini Dar es Salaam.

Alisema tekonolojia ya usafishaji wa maji taka ni muhimu wakati huu taifa likihitaji watu wake kuwajibika ipasavyo kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji  mali kufikia uchumi wa kati kwa njia ya viwanda.

Kwa bahati mbaya, sehemu kubwa ya watu hawajatambua fursa zilizopo katika matumizi ya teknolojia hiyo na kusababisha maji taka yanayozalishwa  kuteketezwa wakati yangetumika kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji wa samaki, ujenzi na bustani.

“Maji machafu ni fursa sio tatizo. Kwa hali ilivyo sasa kila hitaji la maji lazima yatumike maji ya Dawasco. Tunataka maji taka yasafishwe na yatumike kwa shughuli za kuongeza kipato sio kutegemea maji ya Ruvu chini na Juu. Ili kufikia malengo haya ni lazima elimu ipelekwe kwa wananchi ya umuhimu wa teknolojia hizi ambayo pia huzuia magonjwa hasa ya mlipuko,”alisema.
Akifafanua kuhusu mfumo huo wa kutibu maji taka, Nasoro alisema kabla ya maji hayo kutumika hupitia hatua kadhaa kuanzia utengenezaji wa chemba ambayo ni ya kwanza ya matibabu ya maji hayo.

Kisha maji taka hupitishwa kwenye mfumo  wa pili wa tiba unaojulikana kitaalamu kama anaerobic (ABR) na U-Flow Anaerobic (UAF ) ambapo wadudu hula takataka kabla ya kufikia kiwango cha juu cha udhibiti, alisema.

“Maji yanayotibiwa kwa njia hizo yanakuwa yametibika kwa asilimia 85 na kiasi kingine huenda aridhini. Kwa hali hii sio rahisi kusababisha magonjwa, ni salama kwa matumizi kwani yamesafishwa kitaalamu. Yanafaa sana kwa kilimo na ufugaji kwani yana mbolea, nitrogen na phosphorus,”alisema.

Alisema kampuni yake imefanikisha teknolojia hiyo katika taasisi za umma na shule binafsi ya Libermann ya pia ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya maofisa waliotembelea mradi huo kutoka wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,  Jiji la Dar es Salaam na Manispaa za Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo waliridhishwa na utekelezwaji wa mpango huo na kusema hatua inayotakiwa ni jamii kuhamasishwa kujiunga baada ya kuutathimini na kuingizwa kwenye mipango ya ya serikali.

Afisa afya wa Manispaa ya Ubungo Wilson Msangi alisema teknolojia hiyo ni hupunguza gharama ya ukusanyaji wa maji taka, huchukua nafasi ndogo na kushauri Halmashauri kuihamasisha kwenye maeneo kama shule na hospitali kutokana na maeneo hayo kuzalisha kiasi kingi cha maji taka.

`Maji ya chooni ni dili’

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -