Habari Zote
Serikali imelipa madeni
ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha
shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi
Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni halali inayodaiwa na
wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.
Naibu Waziri wa Wizara
ya Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na
badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera
alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na watumishi wa Mamlaka
hiyo.
Hayo yamesemwa Mjini
Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dok. Ashatu Kijaji
(Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika
ziara ya kikazi kukagua utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala
wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
Naibu Waziri wa Wizara
ya Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji
alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
Kijaji alisema kuwa
wazabuni wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2, wakandarasi wamelipwa
shilingi bililioni 24.2, watoa huduma mbalimbali wamelipwa Shilingi bilioni 38,
watumishi wa umma wamelipwa Shilingi bilioni 37, huku wadai wengine wakilipwa
shilingi bilioni 24.
Meneja Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji
ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji
(Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.
Amesema katika bajeti ya
mwaka 2016/2017, Serikali imetenga zaidi ya Shilingi trilioni 1 kwa ajili ya
kulipa madeni mbalimbali na kwamba itaendelea kulipa madeni yote
yaliyohakikiwa.
Baadhi ya Maafisa wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji wa elimu
kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi
hiyo.
Aliiambia Jumuiya ya
Wafanyabiashara mkoani Kagera kwamba Serikali inatambua mchango wao mkubwa
katika maendeleo ya Taifa kutokana na kulipa kodi zinazochangia kuboresha
miundombinu na huduma mbalimbali za jamii.
Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati)
akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa
waadilifu katika kazi zao.
Alitoa wito kwa
wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki katika biashara zao, kutoa
stakabadhi wanapouza bidhaa na huduma huku wananchi wakiaswa kudai stakabadhi
wanapofanya manunuzi ya aina yoyote na kuhakikisha kuwa stakabadhi hizo zinaonesha
kiasi halisi walicholipia huduma na bidhaa walizonunua.
Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati -walioketi) akiwa katika picha ya
pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na
baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Mkoa huo.
Akizungumza kwaniaba ya
Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Seif
Mkude, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna
inavyohamasisha na kushikia bango masuala ya kodi kwa manufaa ya Taifa.
Mwenyekiti wa
Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Seif Mkude (kulia) akielezea kuhusu utayari wa
wafanyabiashara wa Mkoa huo kulipa kodi wakati wa Mkutano kati ya
wafanyabiashara wa Mkoa huo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.
Ashatu Kijaji (Mb) (katikati).
Alisema wafanyabiashara
wameridhika na namna kodi wanazolipa zinavyosimamiwa kikamilifu na kutekeleza
miradi dhahiri ya maendeleo na kuahidi kuwa wataendelea kulipa kodi hizo ili
kujenga uchumi wa nchi.
Mfanyabiashara wa Mkoa
wa Kagera Taimur Manyilizo, akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo
wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile alichoeleza uwepo
wa taasisi nyingi zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto
ambapo aliiomba Serikali iziangalie na kuzifanyia kazi.
Amewashauri kuendelea
kulipa kodi kwa hiari ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli huku akiishauri Serikali kuondoa kero ndogondogo zilizotolewa
na wafanyabiashara wakati wa mkutano huo.
Mfanyabiashara wa Mkoa
wa Kagera Taimur Manyilizo, akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo
wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile alichoeleza uwepo
wa taasisi nyingi zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto
ambapo aliiomba Serikali iziangalie na kuzifanyia kazi.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro, aliwahsa wafanyabiashara
hao kupanua wigo wa biashara zao ili waweze kunufaika na uwepo wa soko huru
katika nchi zaidi ya nne zinazopakana na mkoa huo ikiwemo Uganda, Rwanda,
Burundi, DRC Kongo, Kenya na nchi nyingine.
Imeelezwa kuwa kukamilika kwa Daraja la
Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe kutafufua fursa za kiuchumi
katika mikoa ya magharibi na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na
mifugo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo alipokagua ujenzi wa
daraja hilo na kuwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha daraja hilo linakamilika mwezi Agosti mwakani.
“Toeni ushirikiano unaostahili kwa
mkandarasi ili Daraja hili la Momba na madaraja madogo saba yanayojengwa katika
barabara ya Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa KM 210.38 yakamilike kwa wakati”,
amesema Prof. Mbarawa.
Mafundi wakiendelea na kazi
ya ujenzi wa daraja la Kinambo lililopo katika
barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90
wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
|
Amesisitiza nia ya Serikali ya kujenga
barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 na Stalike-Kilyamatundu-Mloo KM 500
kwa kiwango cha lami ili kuongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa mazao ya
kilimo na mifugo katika Bonde la Mto Rukwa kwenda maeneo mingine ya nchi.
Muonekano wa mitambo ya
kuchimbia nguzo za Daraja la Mto Momba unaounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe.
|
“Wale wote ambao wamewekewa alama za
kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara nawaomba wafanye hivyo mapema
ili kuwawezesha wakandarasi kufanya kazi zao kwa uhuru na kuiwezesha TANROADS
kufanya usanifu wa kina”, alisisitiza.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara
Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina, amemhakikishia Prof. Mbarawa
kuwa watamsimamia kikamilifu mkandarasi anayejenga Daraja la Momba na madaraja
madogo saba katika barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 ili kazi ujenzi
huo ukamilike kwa wakati.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Kwela Ignas Malocha, amewataka wananchi watakaopata fursa za ujenzi wa madaraja
hayo kuepuka vitendo vya wizi na hujuma kwa wakandarasi.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa
Kilymatundu mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Momba,
wilayani Sumbawanga.
Amesema kukamilika kwa Daraja la Momba
kuna manufaa mengi kiuchumi, kijamii kwa kuwa daraja hilo litawaunganisha
wakazi wa jimbo lake na mkoa wa Songwe na hivyo kuharakisha shughuli za
kimaendeleo.
Mmoja wa wananchi wa
kijiji cha Kilyamatundu kilichopo wilayani Sumbawanga akimkabidhi Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ushahidi wa picha za
miti iliyokatwa katika shamba lake kupisha mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto
Momba, mkoani Rukwa.
KUTOKA LONDON,
Kuelekea mchezo wa klabu bingwa balani ulaya leo tarehe 27
usiku wa saa 3:45,viwanja mbalimbali vitalindima ambapo PARIS SAINT GERMAIN
itacheza na BUYEN MUNCHEN,CHELSEA na
ATLETICO MADRID,
pata kufahamu takwimu za mechi zilizokutana kati ya Chelsea vs Atletico Madrid,kutokana na takwimu zilizopo hapo chini ATRETICO MADRID inanafasi kubwa ya kupata ushindi.
pata kufahamu takwimu za mechi zilizokutana kati ya Chelsea vs Atletico Madrid,kutokana na takwimu zilizopo hapo chini ATRETICO MADRID inanafasi kubwa ya kupata ushindi.
Matches
2014-04-30
1
3
2014-04-22
0
0
2012-08-31
1
4
2009-11-04
2
2
2009-10-22
4
0
KUTOKA HISPANIA.
Toleo la kwanza la Kombe la Ulaya lilifanyika wakati wa msimu wa 1955-56.
Timu kumi na sita zilishiriki:
![]() |
| Pichani ni mchezo kati ya Barcelona vs Hamburguliofanyika mwaka 19961 |
Milan (Italia), AGA Aarhus (Denmark), Anderlecht (Ubelgiji), Djurgården (Sweden), Gwardia Warszawa (Poland), Hibernian (Scotland), Partizan (Yugoslavia), PSV Eindhoven (Uholanzi), Rapid Wien ( Austria), Real Madrid (Hispania), Rot-Weiss Essen (Ujerumani Magharibi), Saarbrücken (Saar), Servette (Uswisi).
Uwanja wa Michezo (Portugal), Stade de Reims (Ufaransa) na Vörös Lobogó (Hungary). Mechi ya kwanza ya Kombe la Ulaya ilitokea tarehe 4 Septemba 1955, na ikamalizika kwenye sare ya 3-3 kati ya Sporting CP na Partizan.
Magori ya kwanza katika historia ya Kombe la Ulaya yalifungwa na João Baptista Martins wa CPU katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Parc des Princes kati ya Stade de Reims na Real Madrid, Kikosi cha Madrid kilipata kipigo cha 4-3 ambapo magoli ya Reims yalifungwa na Alfredo DiStéfano,Marquitos, pamoja na magoli mawili kutoka kwa Héctor Rial.
![]() |
Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti
kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
|
![]() |
Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Uchunguzi wa
Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam.
|
![]() |
Profesa Abdulkarim
Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha na Mpiga Picha Maalum
|










