Powered by Blogger.

About

[Michezo kimataifa][column2]

Labels

Search This Blog

[random][featured1]

BTemplates.com

MICHEZO KITAIFA

[michezo][column2]

Blogroll

[afya][fbig2]

Contact us

Name

Email *

Message *

BTemplates.com

Miezi mitatu serikali imelipa Bilioni 190 ya malimbikizo

Serikali imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi ch...

Serikali imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni halali inayodaiwa na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na  watumishi wa Mamlaka hiyo.
Hayo yamesemwa Mjini Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dok. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika  Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
Kijaji alisema kuwa wazabuni wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2, wakandarasi wamelipwa shilingi bililioni 24.2, watoa huduma mbalimbali wamelipwa Shilingi bilioni 38, watumishi wa umma wamelipwa Shilingi bilioni 37, huku wadai wengine wakilipwa shilingi bilioni 24.
 
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.
Amesema katika bajeti ya mwaka 2016/2017, Serikali imetenga zaidi ya Shilingi trilioni 1 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali na kwamba itaendelea kulipa madeni yote yaliyohakikiwa.
 
Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji wa elimu kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi hiyo.
Aliiambia Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera kwamba Serikali inatambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa kutokana na kulipa kodi zinazochangia kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali za jamii.
 
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu katika kazi zao.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki katika biashara zao, kutoa stakabadhi wanapouza bidhaa na huduma huku wananchi wakiaswa kudai stakabadhi wanapofanya manunuzi ya aina yoyote na kuhakikisha kuwa stakabadhi hizo zinaonesha kiasi halisi walicholipia huduma na bidhaa walizonunua.
 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati -walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na baadhi ya Maafisa Waandamizi katika Mkoa huo. 

Akizungumza kwaniaba ya Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Seif Mkude, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna inavyohamasisha na kushikia bango masuala ya kodi kwa manufaa ya Taifa.
 
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Seif Mkude (kulia) akielezea kuhusu utayari wa wafanyabiashara wa Mkoa huo kulipa kodi wakati wa Mkutano kati ya wafanyabiashara wa Mkoa huo na Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati).
Alisema wafanyabiashara wameridhika na namna kodi wanazolipa zinavyosimamiwa kikamilifu na kutekeleza miradi dhahiri ya maendeleo na kuahidi kuwa wataendelea kulipa kodi hizo ili kujenga uchumi wa nchi.
 
Mfanyabiashara wa Mkoa wa Kagera Taimur Manyilizo, akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile alichoeleza uwepo wa  taasisi nyingi zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto ambapo aliiomba Serikali iziangalie na kuzifanyia kazi.
Amewashauri kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huku akiishauri Serikali kuondoa kero ndogondogo zilizotolewa na wafanyabiashara wakati wa mkutano huo.
 
Mfanyabiashara wa Mkoa wa Kagera Taimur Manyilizo, akieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile alichoeleza uwepo wa  taasisi nyingi zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto ambapo aliiomba Serikali iziangalie na kuzifanyia kazi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro, aliwahsa wafanyabiashara hao kupanua wigo wa biashara zao ili waweze kunufaika na uwepo wa soko huru katika nchi zaidi ya nne zinazopakana na mkoa huo ikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, DRC Kongo, Kenya na nchi nyingine.


COMMENTS

[facebook]
Name

AFYA,6,GURUDUMU LA MAISHA,2,HABARI,48,KIJIJINI,7,KIMATAIFA,9,MAHUSIANO NA SAIKOLOJIA,2,MAKALA,2,MAKALA YA ELIMU,1,MICHEZO,2,MIKOANI,4,SARAFU,4,VIDEO,4,ZANZIBAR,1,
ltr
item
LENZI MEDIA: Miezi mitatu serikali imelipa Bilioni 190 ya malimbikizo
Miezi mitatu serikali imelipa Bilioni 190 ya malimbikizo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgU3kSUn38HK9oWEUv4uPIRFHINKbtDyAyam77uhp7LoYG4Bt5DnArVi-p5U-PxkeaAX-5NfuMEr2olkULplybxnfRnTHPne4PJM5cI5gVGOiziWR1mCdqT4HFBCxT-VfYFLLwyKsnzNm0/s640/IMG_1275.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgU3kSUn38HK9oWEUv4uPIRFHINKbtDyAyam77uhp7LoYG4Bt5DnArVi-p5U-PxkeaAX-5NfuMEr2olkULplybxnfRnTHPne4PJM5cI5gVGOiziWR1mCdqT4HFBCxT-VfYFLLwyKsnzNm0/s72-c/IMG_1275.JPG
LENZI MEDIA
https://lenzimedia.blogspot.com/2017/10/miezi-mitatu-serikali-imelipa-bilioni.html
https://lenzimedia.blogspot.com/
https://lenzimedia.blogspot.com/
https://lenzimedia.blogspot.com/2017/10/miezi-mitatu-serikali-imelipa-bilioni.html
true
2372332392983471599
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content