C HAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimetoa mkono wa pole kwa familia iliyopata ajali ya kuungua moto nyumba na kusababisha vifo vya watu w...
CHAMA cha Mapinduzi
(CCM) Zanzibar kimetoa mkono wa pole kwa familia iliyopata ajali ya kuungua
moto nyumba na kusababisha vifo vya watu wanne huko katika kijiji cha Fumba
Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Akizungumza Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Mabodi wakati wa kuifariji familia hiyo
amesema CCM Zanzibar imesikitishwa sana na tukio hilo kwani limegharimu maisha
ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla
Juma Mabodi akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu wa familia iliyopata msiba
huo katika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Dk. Mabodi alisema kwa niaba ya Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki
wa familia hiyo na kuwasihi waendelee kuwa na moyo wa subra katika
kipindi hichi kigumu cha msiba huo.
“ Kupoteza watu Wanne katika familia
moja ni jambo zito linalotia huzuni lakini tuendelee kuwa wavumilivu
kwani Allah amewapenda zaidi na sisi tuliobaki tuendelee kuwaombea dua
ili wapate makaazi mema na kusamehewa madhambi yao”, alitoa nasaha hizo kwa
maskitiko makubwa Dk. Mabodi.”
Mapema Sheha wa Shehia ya Fumba, Mohamed
Suleiman alifafanua kuwa nyumba hiyo ilianza kuwaka moto majira ya saa 6:15
usiku Oktoba 21 mwaka huu, ambapo wananchi mbali mbali walianza juhudi za
kuzima moto huo na kushindwa kuokoa watu waliokuwa ndani kwani uliku ni mkubwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla
Juma Mabodi Akisalimiana na baadhi ya wananchi na viongozi mbali mbali
walioudhuria katika msiba huo.
Suleiman alisema wakati juhudi za kuzima moto
huo zikiendelea waliwasiliana na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar ambacho
kilifika na kusaidiana na wananchi hao ambapo walizima moto huo na kukuta watu
wanne tayari wamefariki dunia.
Akithibitisha tukio tukio hiloalisema chanzo
cha moto huo ni hitilafu za umeme zilizoanzia katika waya wa jokofu (Friji)
lililokuwa likifanya kazi wakati wa usiku.
Kamanda Nassir aliwataja watu waliofariki
katika tukio hilo kuwa ni Bahati Ali Ameir (40), Sinawema Abdalla Ali, Hashim
Abdalla Ali (6) na Latifa Mohamed Ali (8).
Alitoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa
kuzima vifaa vya umeme wakati wa usiku ambavyo havina umuhimu wa kutumiwa
wakati huo ili kuepuka majanga yanayoweza kuhatarisha maisha ya watu.
COMMENTS