AFISA Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsiinafsi wa ...
AFISA Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu
ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule
Binafsiinafsi wa mkoa ikiwemo ya tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule
hizo .
Afisa elimu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na washiriki wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es Salaam |
Pia amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee
kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa kuwa
wana walimu wengi wa masomo hayo.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu
uliowakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa shule zilizopo jijini hapa.
Amesema wamiliki wa shule hizo pamoja na shule zao wanapaswa watambaue
huduma wanazopewa ni stahiki hivyo ni sawa wanazopatiwa shule za
Serikali.
“Natamani kuziona shule zote binafsi zikiwa zinazoongoza kutokuwa na
changamaoto zozote kwani tunatambua mchango wa uwekezaji hapa nchini,” amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Shule
Binafsi nchini (TAMONGSCO), Charles Totela ameishukuru Serikali ya mkoa huo
kwani imekuwa ikiwapa ushirikiano wa kutosha.
Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali ya mkoa huo kuwaundia dawati la
pamoja litakalowakutanisha viongozi wote wa shule binafsi, za serikali na
watendaji wao ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana baadhi ya changamoto ambazo
zimekuwa hazifanyiwi kazi.
Naye Mkurugenzi wa Shule za Al-Muntazir, Mahmood Ladack
amewashukuru wamiliki wa shule hizo kwa kuhitisha mkuatano huo ambao anataraji
utakuwa na manufaa makubwa kwao na taasisi wanazosimamia katika kupambana na
changamoto mbalimbali zinazowakabili.
COMMENTS