Habari Mpya

Habari Zote

Archive for August 2022

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewakumbusha wananchi wa kijiji cha Vuchamangofi wanaohitaji kuwekewa umeme gharama zake ni Sh. 27,000 kwa vna sio vinginevyo kama ambavyo wamekuwa wakidanganywa


"Msikubali kutozwa zaidi ya Sh.27,000 kwa sasa umeme sio hanasa, kila mtu anatakiwa kupata huduma hii kwa gharama ya chini kwa sababu serikali imeamua kutoa huduma hii maeneo yote nchini," amesisitiza Chongolo.

Chongolo ameyasema hayo akiwa wilani Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa kwenye mwendelezo wa ziara ya siku tano ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, miradi ya maendeleo na kuhimiza sensa ya watu na makazi

Amesema kuna watendaji wasio waaminifu wanawalaghai wananchi kulipa zaidi ya kiasi hicho.



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua maofisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa mujibu wataarifa iliyotolewa usiku wa Jumamosi, Agosti 6, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus amefanya uteuzi huo juzi Alhamisi Agosti 4, 2022.



Miongoni mwa walioteuliwa kuwa majaji wa Mahakama Kuu ni pamoja na Gabriel Pascal Malata ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Kevin Mhina.

Majaji hao walioteuliwa ambao tarehe ya kuapishwa itatangazwa ni;

1. Kevin David Mhina- kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani

2. Gabriel Pascal Malata-kabla ya uteuzi huu alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali

3. Adrian Philbert Kilimi- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili Mahakama

4. Happiness Philemon Ndesamburo- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

5. Victoria Mlonganile Nongwa- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

6. Obadia Festo Bwegoge- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

7. Ruth Betwel Massam-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

8. Godfrey Ntemi Isaya-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

9. Gladys Nancy Barthy-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

10. Haji Suleiman Haji- kabla ya uteuzi alikuwa Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar

11. Fatma Rashid Khalfan-kabla ya uteuzi alikuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

12. Abubakar A. Mrisha-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Serikali

13. Lusungu Hemed Hongoli-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

14. Monica Peter Otaru-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

15. Kamana Stanley Kamana-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi (Tamisemi)

 16. Hamidu Rajabu Mwanga-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi

17. Marlin Leonce Komba-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

18. Dk Mwajuma Kadilu Juma-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe

19. Dk Cleophas K.K. Morris-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam

20. Asina A. Omani-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

21. Aisha Zumo Bade- kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea

22. Mussa Kassim Pomo-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Taarifa hiyo imesema kuwa tarehe ya kuapishwa majaji hao wateule itatangazwa baaadaaye.


RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na maji katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Amesema anatambua matatizo yanayowakabili kina mama kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu hivyo Serikali itahahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 tatizo la maji nchini linakuwa limekwisha.

Rais Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji wa Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizindua mradi wa maji katika kata ya Makongorosi Wilaya ya Chunya wenye thamani ya Sh2.5 bilioni utakaozalisha maji lita Milioni mbili kwa siku.

 

Amesema katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ifikapo 2025 ilielekeza kutatua tatizo la maji na kwa Mkoa wa Mbeya kuna miradi 50 ambayo imefikia asilimia 95 na ifikapo 2025 tatizo la maji litakwisha kwa asilimia 100.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athon Sanga amesema mradi huo umefikia asilimia 70 ambao utazalisha lita milioni mbili zitakazo ondoa tatizo la maji katika Wilaya ua Chunya.

 

Amesema wizara ina mpango wa kuchimba visima vikubwa vya maji  katika mji wa Makongorosi ili kuondokana na hadha kwa baadhi ya maeneo huku akimpongeza  Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka kwa kutatua changamoto ya maji jimboni kwake kwa kuchimba visima.

 

Kwa upande wake, Mbunge Kasaka amemuomba Rais Samia kusaidia kuboreshwa miundombinu ya barabara kutoka chunya mpaka kijiji cha Itumbi ambako kuna shughuli za uchimbaji wa madini ili kufungua fursa za kiuchumi.

 

Mchimbaji mdogo wa Madini Kata ya Matundasi, Aden Mwakyusa amesema ujio wa Rais Samia ikawe chachu ya changamoto za wachimbaji madini kutatuliwa pamoja na kuhodhi maeneo ambayo yanashikiliwa na wachimbaji wakubwa.

CHANZO MWANANCHI

 

WAZIRI mkuu wa Tanzania KASSIM MAJALIWA amezindua mradi unaofahamika kama farm clinic wenye lengo la kuwezeshwa wakulima kufikia ajenda ya 10/30 yenye kauli mbiu ya kilimo ni biashara kupitia farm clinic.

MAJALIWA amefanya uzinduzi huo alipo tembelea maonesho ya nane nane jijini Mbeya huku akiwahimiza vijana kuingia kwenye sekta ya kilimo kwa kuwa serikali imeandaa mipango mingi na mizuri kwa ajiri yao.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa


MAJALIWA amesema kuwa anaomba kila mwananchi ajishughulishe na shughuli ambayo itamleta uchumi ambayo itamsaidia kupata kipato ambacho kitamsaidia kila mtanzania kuendesha familia.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mbeya mjini na spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania TULIA ACKSONI MWANSASU ametumia nafasi hiyo hiyo kumshukuru rais samia suruhu hassani kwa kuleta mradi mkubwa wa maji ambao unaenda kumaliza changamoto ya maji jijini Mbeya.

NA: ANYIGULILE ZAKARIA


 

SERIKALI ya kijiji cha Lulembela wilayani Mbogwe Mkoani Geita imewatahadharisha baadhi ya watu wenye tabia ya kuwaficha watoto kisha kuanza kudai fidia kwa wazazi wao kwa kisingizio walikuwa wamepotea.

Kaimu Afisa Mtendaji Wa kijiji hicho PAUL NTAHENGAMA ametoa tahadhari kwa watu wenye tabia hiyo nakwamba wamekuwa wakipata taarifa kutoka kwa wananchi japo hawajabaini juu ya uwepo wa vitendo hivyo kwani wengi wanaowakota watoto hao huwaokota kwa nia njema na si kwa biashara.



kwa mujibu wa maelezo ya wananchi katika Eneo hilo wamedai wimbi la kupotea watoto kwa sasa ni kubwa nakwamba cha kushangaza pindi wanapowapata watoto hao huwalazimu kutoa fidia kuwakomboa kutoka kwa wasamalia wema waliowaokota jambo Ambalo wamehisi huenda kuna biashara ambayo inaendelea. Moja kati ya mzazi ambae amekumbana na changamoto ya mtoto wake kupotea nakulipishwa fidia amesema.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho MAISHA WILLIAM MAGINYA amesema Uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha watu wanaotumia Fursa hiyo ya kuficha watoto kujiingizia  kipato wameendelea kulifanyia kazi ili kubaini uwepo wa vitendo hivyo.

Katika hatua Nyingine Bw William amewataka wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao ili kuondokana na changamoto kama hizo kwakuwa wazazi wengi wamekuwa bize na uzalishaji mali nakusahau malezi kwa watoto.

NA NICHORAS PAUL LYANKANDO

BAADHI ya wafanyabiashara katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani geita  mkoani Geita wamesema sheria kandamizi za ulipaji wa kodi imekuwa kisababishi cha wengi wao kuingia katika vishawishi vya utoaji wa rushwa ili kuendelea na biashara.

Wakizungumza katika moja ya kikao na maafisa wa Mamlaka ya Mapato TRA Wafanyabiashara hao wametoa malalamiko yao juu Sheria kandamizi Ambazo zinawakandamiza wafanyabiashara.



Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara CHARLES MAKANJI amesema TRA wamegeuka kuwa chanzo cha kuwadidimiza wafanyabiashara kwa kuwatoza faini Ambazo haziendani na mitaji yao.

Akitoa Ufafanuzi wa suala la kodi Mwalimu Toa Elimu ya Kodi kanda ya ziwa LUTUFYA MTAFYA amesema wao wanasimamia Sheria na Hawamkandamizi mfanyabiashara hivyo amewaomba wawasilishe kero zao katika Ofisi za mamlaka hiyo na kero zao kutatuliwa haraka iwezekenavyo.

Katika Hatua nyingine akawaomba kutoziogopa Ofisi za TRA badala yake watumie ofisi hizo kama kimbilio la kwanza kutatuliwa kero zao.

NA NICHORAS PAUL LYANKANDO



 

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha CNL Agathon Rwasa amesema kupunguzwa kwa mikoa haitakuwa suluhu ya migogoro ya uchaguzi nchini.

NA: BUKURU ELIAS, RWASSA

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -